Saturday , 11 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Makamba atua Algeria kushiriki mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje
Habari za Siasa

Makamba atua Algeria kushiriki mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje

Spread the love

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amewasili nchini Algeria kushiriki Mkutano wa 20 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Nordic utakaofanyika tarehe 16 – 18 Oktoba 2023, Jijini Algiers, Algeria. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mara baada ya kuwasili nchini Algeria, Makamba alipokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Houari Boumediene Jijini Algiers na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Diaspora ya Algeria, Lounes Magramane.

Mkutano wa 20 wa nchi za Afrika na Nordic unahusisha nchi tano za Nordic ambazo ni Finland, Sweden, Denmark, Norway na Iceland pamoja na nchi 25 za Afrika ambazo ni marafiki (wenye ushirikiano na Nordic) wa Nordic.

Mkutano kati ya nchi za Afrika na Nordic ulianza mwaka 2000 ambapo mwaka 2001 Mkutano wa kwanza ulifanyika nchini Sweden na imekuwa ikifanyika kwa kupokezana kati ya nchi za Nordic na Bara la Afrika.

Itakumbukwa kuwa Tanzania ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa 18 kati ya Nordic na Afrika mwaka 2019 ambapo nchi 34 zilishiriki katika mkutano huo.

Tanzania ni moja kati ya marafiki wakubwa wa nchi za Nordic na imekuwa ikishiriki mikutano ya Afrika – Nordic inapokuwa ikifanyika.  Mkutano wa mwaka 2022 kati ya Nchi za Afrika na Nordic ulifanyika mwezi Juni 2022 Helsink, nchini Finland.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina awavaa mawaziri wanaompelekea majungu Rais Samia

Spread the loveMBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amewataka baadhi ya mawaziri...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

THRDC, Wizara ya Katiba wajadili uanzishaji haki binadamu katika biashara

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umefanya...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Sitta ang’ang’ana wanafunzi watibiwe bure, Serikali yagoma

Spread the loveMBUNGE wa Urambo, Margaret Sitta, ameishauri Serikali iweke utaratibu wanafunzi...

error: Content is protected !!