Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Makala: Puuzeni wanasiasa wanaojigamba wanaweza kubadili maamuzi ya mahakama
Habari za Siasa

Makala: Puuzeni wanasiasa wanaojigamba wanaweza kubadili maamuzi ya mahakama

Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Amos Makala
Spread the love

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makala, amewataka wananchi wenye madai ya haki ambayo hayajafikishwa mahakamani kuwasilisha migogoro yao kwa viongozi wa chama hicho ili wapate msaada. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza katika mkutano wa viongozi wa CCM mkoani Katavi, leo Jumamosi, Makala amewataka wananchi kupuuza wanasiasa wanaowaeleza kwamba wana uwezo wa kubadili maamuzi ya mahakama.

“Changamoto za Katavi nazijua, unaambiwa hili liko mahakamani, asije mwanasiasa akakudanyanga kwamba anaouwezo wa kubadili maamuzi ya mahakama akakupa haki, wote tunaamini kwamba chombo ambacho kikatiba cha kutoa haki ni mahakama,” amesema Makala na kuongeza:

“Sisi tuko tayari kusikiliza kero zozote ambazo bado hazijaingia kwenye mhimili wa mahakama, tutawasaidia wananchi wanyonge katika mambo ambayo bado hayajaingia katika mahakama ili apate haki hiyo na wale ambao wako mahakamani ushauri mkubwa kama ulikosa haki mahakama ya chini ukate rufaa mahakama ya juu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!