Monday , 13 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Makada 6 CCM wafariki kwa ajali
Habari za Siasa

Makada 6 CCM wafariki kwa ajali

Spread the love

Viongozi sita wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamefariki dunia na wengine 11 kujeruhiwa katika ajali ya gari ya abiria Toyota Haisi lenye namba za usajili T 733 BBP baada ya kupinduka katika kijiji cha Ndulamo wilaya ya Makete mkoani Njombe. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Jumamosi baada ya dereva wa gari hilo kushindwa kukata kona.

RPC Njombe -John Imori

Aidha, pia imeelezwa kuwa makada hao walikuwa wakitoka kwenye mkutano wa mlezi wa chama hicho mkoa wa Njombe, Halima Mohamed Mamuya uliyokuwa ukifanyika wilayani humo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe John Makuri Imori amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo katika ajali ya gari hiyo iliyokuwa ikitokea Makete kuelekea Tandala.

Amesema katika gari hilo lililokuwa na abiria 18, kati ya sita waliofariki, watatu ni wanaume na watatu ni wanawake).

Ameongeza kuwa chanzo cha ajali ni mwendokasi uliomfaya dereva kushindwa kulimudu gari hilo lililokuwa katika mteremko mkali.

Aidha, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Juma Mfanga amesema majeruhi wengi wamevunjika viungo na wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Ikonda.

Amesema wengine wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Makete ambapo pia tayari madaktari wengine kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe wamefika katika Hospitali hizo kuongeza nguvu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Wizara afya kutumia Sh. 1.31 trilioni, huduma za kibingwa zapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Afya, imeliomba Bunge lipitishe makadirio yake ya mapato...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wizara kutumia Sh. 3.5 bilioni kuchunguza afya ya akili, nguvu za kiume

Spread the loveWIZARA ya Afya, imepanga kutumia Sh. 3.50 bilioni, kwa ajili...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

THRDC yapaza sauti changamoto ya intaneti

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umeitaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Prof. Ndakidemi aitaka TMA kutoa taarifa kwa njia ya SMS

Spread the loveMBUNGE wa Moshi Vijijini, Profesa Patrick Ndakidemi (CCM) ameishauri Serikali...

error: Content is protected !!