Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maelfu wampokea Rais Samia Manyara, viongozi wa dini wanena
Habari za Siasa

Maelfu wampokea Rais Samia Manyara, viongozi wa dini wanena

Spread the love

MAELFU ya wananchi mkoani Manyara, wamejitokea kumpokea Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ili kumuunga mkono kwa kazi kubwa anayofanya kuleta maendeleo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Manyara…(endelea).

Wananchi hao wamejitokea katika uwanja mpya wa Manyara wa Tanzanite Kwaraa, leo tarehe 14 Oktoba 2023, ambapo RaiS Samia anafunga kilele cha mbio za mwenge wa uhuru.

Maelfu ya wananchi Manyara, leo Jumamosi wamejitokeza katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, kwa ajili ya kumuunga mkono Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kazi anazofanya kuleta maendeleo.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, amesema mwitikio mkubwa wa wananchi kushiriki katika hafla hiyo, ni kutokana na kuridhishwa na utendaji wa Serikali ya Rais Samia, huku akisema wengi wao wamefika kwa ajili ya kumshukuru.

Sendiga amesema tangu ameingia madarakani Machi 2021, Serikali yake imepeleka mkoani humo kiasi cha Sh. 535.7 bilioni.

“Kipindi hiki kifupi fedha hizi zimekwenda kwenye miradi ya maendeleo na wananchi wengi wamekuja kukuona ili waweze kukushuru,” amesema Sendiga.

Katika hatua nyingine, Sendiga amesema tukio la kuzimwa Mwenge pamoja na maadhimisho ya wiki ya vijana, yamechochea uchumi wa mkoa huo.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Pentekoste Tanzania na Mwenyekiti wa Viongozi wa Dini Manyara, Peter Konki amesema ujio wa Rais Samia mkoani humo ni Baraka.

“Namtambua Rais Samia kama kiongozi mwenye juhudi na nguvu, hata wakati anaanza watu walikuwa wanauliza maswali lakini niliwaambia mwanamke ni mtu imara sana kwenye utendaji na kwa tabia ya mwanamke hapendi kushindwa na ameonyesha hilo hapendi kushinfwa na hapendi aibu,” amesema Askofu Konki na kuongeza:

“Yale ambayo Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere alikuwa anayatamani ilikuwa uhuru wa wananchi ambayo mama anapambana nayo watu wamekuwa huru kutoa maoni yao mpaka wanapitiliza. Amekuwa kiongozi mvumilivu.”

kwa upande wake Sheikh wa Mkoa wa Manyara, amewataka watanzania wamuombee Rais Samia kwa Mungu ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

“Tunayo furaha kubwa sana Rais Samia kuja Manyara, tunamuomba Mwenyezi amhifadhi na ampe afya njema ili azidi kutupigania” alisema Sheikh Mohamed H. Kadidi

Sambamba na hilo, Sheikh wa Mkoa wa Manyara amempongeza Rais Samia kwa kwa kuishi ndoto za Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu, Julius Kambarage katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo na uzalendo wake kwa Taifa letu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

ACT-Wazalendo yasusia uchaguzi wa ubunge Zanzibar

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo, kimegoma kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo...

error: Content is protected !!