Tuesday , 30 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Majaliwa: Mh. Rais, naanza na saruji
Habari za Siasa

Majaliwa: Mh. Rais, naanza na saruji

Spread the love

KASSIM Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania, ameagiza maofisa wa wizara yake na wakuu wa mikoa kwenda katika viwanda vya uzalishaji saruji, kujua sababu za bidhaa hiyo kupanda ‘kienyeji’. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Amewataka maofisa hao kufika kwenye viwanda mbalimbali nchini tarehe 20 Novemba 2020, saa nne asubuhi, ili kupata maelezo kuhusu sababu za bidhaa hiyo kupanda sokoni.

Akizungumza mbele ya Rais John Magufuli baada ya kuapishwa kuwa Waziri Mkuu katika viwanja vya Ikulu, Chamwino jijini Dodoma, Waziri Majaliwa amehoji, sababu za bei ya saruji kupanda wakati Serikali haijapandisha kodi, makaa ya mawe wala kujafanya mabadiliko yoyote.

“Kuna upandaji wa saruji bila sababu za msingi, miaka mitano iliyopita tulijenga mazingira ya baiashara kuwa rahisi. Hatukutarajia saruji kupanda, mheshimiwa rais (Rais Magufuli) naaanza na hilo.”

“Tarehe 20 saa nne asubuhi, maofisa wangu waende kwenye viwanda kujua kwanini saruji imepanda wakati serikali haijapandisha kodi, makaa ya mawe. Tunahitaji maelezo kwanini bei ya saruji imepanda kwa kiasi hicho,” amesema Majalia.
Waziri Majali amesema, kwa kuwa moja ya kazi yake kubwa ni kuhakikisha malengo ya Serikali na ilana ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2020 – 2025 inatimia, atapita kila wizara kusisitiza hilo.
“…nitapita kila wizara kuhakikisha mipango na ilani inatekelezwa, hilo ndio jukumu kubwa linaanza”

Pia, Waziri Majaliwa amewashukuru wabunge kwa kuridhia jina lake kuwa Waziri Mkuu akisema, tabia yake ni ile ile ya kuwasikiliza na kuwahudumia wabunge kwa maslahi ya Taifa.

“Nawashukuru wabunge wenzangu baadhi ya uthibitisho uliopelekwa bungeni, pia nashukuru kwa kunishindikiza. Ni matarajio yetu wakati wote tukiwa kwenye majukumu yetu tutatenda yale Watanzania wanatarajia.”

“Bado msimamo wangu ni ule ule wa kuwapokea, kuwasikiliza na kuwahudimia wabunge. Ni jukumu langu kuhakiklisha malengo yaliyowekwa na ilani ya uchaguzi yanakamilika,” amesema.

Mbali na Waziri Majaliwa kuapishwa, wengine walioapishwa ni Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pia Dk. Philip Mpango, Waziri wa Fedha.

Baadhi ya wageni waliohudhulia ni; Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, Spika wa Bunge, Job Ndugai na Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma.

Wengine ni; Maspika wastaafu; Pius Msekwa na Anne Makinda; Mawaziri wakuu wastaafu; John Malechela, Frederick Sumaye, Edward Lowassa na Mizengo Pinda. Wakuu wote wa mikoa, makatibu wakuu wote wa wizara, wabunge wa Bunge la 12.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

7 wafa Ulanga, mbunge alia kutelekezwa na mawaziri, Tanroad

Spread the loveWatoto saba wamepoteza maisha na zaidi ya kaya 70 kukosa...

Habari za SiasaTangulizi

Wizara Katiba na Sheria yaliomba Bunge Sh. 441.2 bilioni

Spread the love  WIZARA ya Katiba na Sheria imeliomba Bunge liidhinishe bajeti...

error: Content is protected !!