Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Majaliwa: Hakuna wakupinga Tanzania ilikuwa kinara ukombozi Afrika
Habari za Siasa

Majaliwa: Hakuna wakupinga Tanzania ilikuwa kinara ukombozi Afrika

Spread the love

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema hakuna wa kupinga kluwa Tanzania chini ya uongozi wa Hayati Mwl. Julius Nyerere, ilikuwa kinara wa ukombozi wa bara la Afrika dhidi ya ukoloni. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Majaliwa ameyasema hayo leo Jumamosi tarehe 23 Aprili, 2022 wakati akizungumza katika sherehe za kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa Mwl. Nyerere zilizofanyika Msasani Jijini Dar es Salaam.

Amesema ni katika kipindi cha uongozi wake Tanzania ilikuwa kitovu cha ukombozi wa nchi za kusini mwa bara la Afrika ikiwa makao makuu ya kamati ya ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika, “harakati nyingi zilianzia hapa nchi na kuenea kwingineko barani Afrika.”

Amesema Tanzania ilitoa na kutenga maeneo ya nchi yake kwaajili ya ujenzi wa kambi, ofisi, vyuo vya mafunzo na nyumba za makazi, “hadi pale ilipohakikisha bara la Afrika linabaki kuwa huru,”

Ameongeza kuwa baadhi ya viongozi wa Afrika waliongoza mapambano dhidi ya ukombozi wa nchi zao, waliishi na kuratibu mapambano dhidi ya ukoloni wakitokea Tanzania.

“Kwa mantiki hiyo hakuna mwenye uwezo wa kupinga kuwa tanznaia chini ya uongozi wa Mwl. Nyerere ilikuwa kinara wa ukombozi wa bara la Afrika,” alisema.

Amesema misingi ya waasisi wa Taifa imekuwa sababu ya uhuru, utu, amani, heshjima, utulivu umoja wa kitaifa demokrasia na maendeleo tunayoshuhudia leo.

“Kwa misingi hiyo tunayo kila sababu ya kuendela kukumbuka na kuenzi juhudi za misingi hiyo ambayo sit u ilitutoa katika minyororo ya kutawalia na wakoloni bali ziliasisi taifa imara ambalo tunajivunia leo hii,” amesema Majaliwa.

Aliwashukuru wazee ambao wanashirikiana na wanazuoni kuelezea maisha ya Mwl. Nyerere yaliyojaa utumishi wa kutukuka kwa taifa.

“Wengine walifuikia hatua ya kuandika vitabu na hivyio kutuachia urithi usio na kifani kwa kizazi cha sasa na vijavyo,” amesema Majaliwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!