Friday , 10 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Majaliwa azindua kampeni ya Mama Samia, atembelea banda la NMB
Habari Mchanganyiko

Majaliwa azindua kampeni ya Mama Samia, atembelea banda la NMB

Spread the love

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuitumia kampeni ya Huduma ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia kutoa taarifa kuhusu uwepo wa watu au vikundi vya watu ambao ama wanajihusisha na ukatili wa kijinsia hususan kwa watoto. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Majaliwa alitoa wito huo Alhamisi tarehe 27 Aprili 2023 alipozindua kampeni hiyo ambayo itatekelezwa kwa miaka mitatu kuanzia Machi, 2023 hadi Desemba 2025.

Katika uzinduzi huo, Majaliwa alitembelea mabanda mbalimbali ikiwemo la Benki ya NMB na kuzungumza na wafanyakazi wa benki hiyo akiwemo, Mkuu wa Idara ya Huduma za Serikali wa Benki Ya NMB, Vicky Bishubo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Idara ya Huduma za Serikali wa Benki Ya NMB, Vicky Bishubo ( kushoto) alipotembelea Banda la Benki hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya “Mama Samia legal Aid” yenye lengo la kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi hususani walio maeneo ya pembezoni. Wapili kulia ni Waziri wa Katiba na sheria, Dkt. Damas Ndumbaro na wengine ni watumishi wa Benki ya NMB.

Majaliwa alisema kampeni hiyo itasaidia kuongeza uelewa wa sheria na upatikanaji haki, mifumo ya utoaji haki, masuala ya kisheria na haki za binadamu kwa kushirikiana na taasisi za serikali, asasi za kiraia na wadau wa maendeleo katika utoaji huduma kwa wananchi.

“Kampeni hii pia itasaidia kuboresha upatikanaji wa haki kwa watu wasiojiweza, hususani wanawake, watoto na makundi mengine yaliyo katika mazingira magumu. Vilevile, itachangia kuimarisha amani na utulivu, kuongeza kipato cha mmoja mmoja na kuleta utengamano wa kitaifa,” alisema.

Aliongeza faida nyingine ya kampeni hiyo ni kusaidia kuimarisha mfumo wa utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria katika ngazi zote yaani kuanzia Serikali kuu hadi Serikali za Mitaa.

“Ushiriki wa wadau wanaojihusisha na huduma ya msaada wa kisheria utaongezeka kwa asilimia 80 katika ngazi za Serikali Kuu hadi Serikali za Mitaa,” alisema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliiagiza Wizara ya Katiba na Sheria iweke mfumo mzuri wa kushughulikia changamoto za kisheria zitakazoibuliwa wakati wa Kampeni katika utimilifu wake.

“Tusiache wananchi wakiwa bado hawajapata majibu ya changamoto zao. Hii itasaidia kujenga taswira nzuri kwa Serikali wala kwa mamlaka ambayo imeridhia kuwepo kwa Kampeni hii,” alisema

Kadhalika, Majaliwa ameitaka Wizara hiyo itekeleze majukumu yake kwa ufanisi na weledi mkubwa ili Watanzania wote waweze kuifikia haki na kuipata haki  kwa wakati.

“Kwa wale ambao hawawezi kumudu gharama za mawakili wa kujitegemea hakikisheni wanapata huduma za kisheria bila ya upendeleo wowote na kwa viwango stahiki”.

Kwa upande wake, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro alisema kampeni hiyo ambayo ni maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wanatoa elimu ya sheria na kusaidia wahitaji ndani ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, wamepanga kutoa elimu katika maeneo ya migogoro ya Ardhi, mirathi, ndoa, sheria ya mtoto katika maeneo ya Ukatili wa kijinsia na Maadili.

Alisema kampeni hiyo itatekelezwa pande zote mbili za Muungano kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Serikali na wasio wa serikali ikiwemo Ofisiya Mashtaka, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ustawi wa Jamii, vyuo vya elimu ya juu,

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

THRDC, Wizara ya Katiba wajadili uanzishaji haki binadamu katika biashara

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umefanya...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Sitta ang’ang’ana wanafunzi watibiwe bure, Serikali yagoma

Spread the loveMBUNGE wa Urambo, Margaret Sitta, ameishauri Serikali iweke utaratibu wanafunzi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Waitara ahoji bungeni mwarobaini mauaji katika mgodi Barick North Mara

Spread the loveMBUNGE wa Tarime Vijijini (CCM), Mwita Waitara, ameitaka Serikali kutafuta...

error: Content is protected !!