Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Majaliwa amtembelea Mbowe hospitalini 
Habari za Siasa

Majaliwa amtembelea Mbowe hospitalini 

Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa (aliyesimama) akimjulia hali Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amemtembelea na kumjulia hali Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe ambaye amelazwa katika hospitali ya Ntyuka jijini Dodoma kwa matibabu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Chadema, amelazwa hospitalini hapo baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana usiku wa kumakia leo Jumanne tarehe 9 Juni 2020 na kumvunja mguu wa kulia.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu imesema, Majaliwa amemuombea kiongozi huyo uponyaji wa haraka wa majeraha aliyoyapata.

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa  taarifa za tukio la kuvamiwa kwa mheshimiwa Mbowe na watu ambao bado hawajajulikana, namuomba Mwenyezi Mungu amjalie  apone haraka ili aweze kurejea katika majukumu yake,” amesema Majaliwa

Baadhi ya wabunge wa upinzani waliokuwepo hospitalini hapo na ambao walimpokea Waziri Mkuu ni Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya, Mbunge Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!