Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko TYC ‘yalilia’ uchaguzi shirikishi Tanzania  
Habari Mchanganyiko

TYC ‘yalilia’ uchaguzi shirikishi Tanzania  

Mshauri Mwelekezi wa TYC, Zatwa Nyingi 
Spread the love

WAKATI  maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020 yakiendelea nchini Tanzania, Shirika lisilo la Kiserikali la Tanzania Youth Coalition (TYC) limetaka kufanyika kwa majadiliano baina ya wadau wote wanaohusisha uchaguzi huo ili kujenga umoja. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea)

TYC imesema, kilichotokea katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika tarehe 24 Novemba 2019 kimeacha majeraha kwa baadhi ya makundi hivyo, kuingia kwenye uchaguzi mkuu pasina kuyatibu ni tatizo.

Shirika hilo ambalo linafanya chini ya mwamvuli wa Ushiriki Tanzania limesema hayo leo Jumanne tarehe 9 Juni 2020 wakati wakitoa tathimini ya utafiti walioufanya kwa wilaya za Ubungo na Kinondoni jijini Dar es Salaam jinsi wanawake, vijana na wenye ulemavu walivyoshiriki uchaguzi huo.

Mshauri Mwelekezi wa TYC, Zatwa Nyingi amesema, katika uchaguzi huo wa serikali za mitaa, baadhi ya vyama havikushiriki jambo lililosababisha wagombea wengi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupita bila kupingwa.

Amesema, ili yasije kujirudia ya uchaguzi wa serikali za mitaa katika uchaguzi mkuu ujao, ni wakati wa wadau wa uchaguzi kama Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), vyama vya siasa na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

“Tungependa sana, tunapoingia katika uchaguzi ujao, tumejeruhiana kwa namna moja au nyingine, makundi ya watu wenye ulemavu, vijana, wanawake, NEC, Tamisemi na vyama vya siasa wakae pamoja wajadiliane ili kuwa na uchaguzi shirikishi,” amesema

Amesema, katika utafiti huo mdogo, wamebaini makundi ya wanawake, vijana na wenye ulemavu yamekuwa hayapewi kipaumbele, “na kama wanashirikishwa, wanapewa ushirikiano dakika za mwisho hali inayowafanya wasifanikiwe kuwa washiriki makini.”

Nyingi amesema, waliamua kufanya utafiti huo Kigamboni na Ubungo kwa sababi ni wilaya mpya ambazo zinawakirisha maeneo mengine nchini.

Pia, Nyingi amesema, makada mbalimbali wa vyama vya siasa pamoja na asasi za kiraia kuhakikisha wanatoa elimu kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu ili kuwahamasisha umuhimu wa kushiriki kwenye uchaguzi ikiwemo kugombea  kwenye nafasi kama za udiwani, ubunge na Urais.

Naye Mkurugenzi wa TYC, Lenin Kazoba amesema, lengo ni kuona namna gani ushiriki wa wanawake, vijana na wenye ulemavu unakuwa mkubwa, “na kipi cha kujifunza ili tusirudie makosa ambayo yanajitokeza kwani ushiriki wa vijana katika vyama vya siasa umekuwa mfinyu.”

Kazoba amesem, bado kuna nafasi kubwa kwa makundi haya kushirikishwa kuanzia hatua za mwanzo kabisa za uchukuaji fomu na urejeshaji ili kuwa na uwiano sawa.

Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Rose Reuben

“Kwani hayapewi mwamko mapema, mfano mtu akitaka kuchukua fomu anaanzia wapi, hii imekuwa ni siri,  sasa tunataka wanawake, vijana na wenye ulemavu washirikishwe ipasavyo.”

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Rose Reuben ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa Ushiriki Tanzania inayounda mashika 23 amesema, makundi hayo ya wanawake, vijana na wenye ulemavu yanapaswa kupewa kipaumbele kama wengine.

“Vyama vya siasa ndiyo chanzo cha kupatikana kwa washiriki wa uchaguzi, kwa hiyo ni wakati sasa wa kutoa fursa kwa makundi yote, kwa usawa bila kubagua ili tuwe na viongozi wanawake, vijana na wenye ulemavu,” amesema Rose

“Tunawaomba viongozi wa vyama walifanyie kazi hili na inawezekana kwani baada ya makosa ya nyuma ni wakati wa kusonga mbele na kuwa na usawa na ushirikishi wa makundi yote,” amesema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!