Tuesday , 26 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Majaliwa amkaribisha Biteko ofisini, ampongeza kwa kuaminiwa
Habari za SiasaTangulizi

Majaliwa amkaribisha Biteko ofisini, ampongeza kwa kuaminiwa

Spread the love

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo tarehe 2 Septemba 2023 amemkaribisha Naibu Waziri Mkuu Dkt. Doto Biteko katika ofisi ndogo ya Waziri Mkuu zilizopo Magogoni jijini Dar es Salaam na amemuahidi kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuiongezea nguvu Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kumteua Mheshimiwa Dk. Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu ili waweze kusimamia uratibu shughuli za Serikali kwa pamoja.


“…Kwa niaba yenu Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu tunakukaribisha sana hapa katika ofisi yetu na tunakupongeza kwa kuaminiwa na Mheshimiwa Rais kupewa jukumu kubwa la Naibu Waziri Mkuu kwa lengo la kusimamia shughuli za Serikali. Nakuhakikishia kwamba una timu imara ambayo inatoa ushirikiano wakato wote.”

Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu amemshukuru Rais Samia kwa kumuamini na kumteua kushika wadhifa huo na ameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano. Amewaomba watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wafanye kazi kwa bidii ili maono ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia na watanzania yaweze kufikiwa.

Viongozi wengine walioshiriki mapokezi hayo ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako.

Wengine ni Naibu Waziri Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi, Katibu Mkuu ofisi ya Waziri wa Nchi Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Syprian Luhemeja na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Habari za Siasa

Kamugisha aanika utekelezaji mpango kazi 2022/23

Spread the loveMWENYEKITI wa Ngome ya Vijana ya Chama Cha ACT-Wazalendo Mkoa...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo wakabidhiwa kivumbi kulinda kura uchaguzi 2024,2025

Spread the loveNGOME ya Vijana ya Chama cha  ACT-Wazalendo, imetakiwa kuwanoa wafuasi...

error: Content is protected !!