Tuesday , 7 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mahakama yapinga ombi la Trump la kuondolewa mashtaka ya ubakaji
Kimataifa

Mahakama yapinga ombi la Trump la kuondolewa mashtaka ya ubakaji

Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump
Spread the love

 

JAJI mmoja wa mahakama ya serikali mjini New York nchini Marekani ametupilia mbali juhudi za rais wa zamani wa nchi hiyo, Donald Trump za kuondolewa mashtaka ya ubakaji yaliyowasilishwa na mwandishi E, Jean Carroll, kwamba alimharibia jina kwa kupinga kwamba hakufanya hivyo katikati ya miaka ya 90. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Jaji Lewis Kaplan akiwa kwenye mahakama ya Manhattan, New York, amepinga ombi la Trump kwamba alikuwa analindwa dhidi ya mashtaka kutokana na cheo chake cha urais.

Trump alidai kwamba Carroll alisubiri kwa miongo kadhaa kabla ya kuwasilisha malalamiko yake hivyo ilimlazimu kujitetea.

Hata hivyo, Mawakili wa Trump na Carroll hawajasema lolote kutokana na uamuzi huo.

Carroll alifunguka mara ya kwanza hapo Juni 2019, pale aliposhtumu Trump kwamba alimshambulia kwenye chumba cha kujaribia mavazi kwenye duka la Bergdorf Goodman, kwenye kitongoji cha Manhattan.

Hata hivyo, Trump alikanusha kumfahamu na kusema kwamba Carroll hakuwa aina ya wanawake awapendao.

Carroll anaomba kulipwa ridhaa ya takriban dola Marekani milioni 10, na kesi yenyewe imepangwa kusikilizwa tarehe 15 Januari mwaka ujao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!