Saturday , 4 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mshahara wa milioni 28 kwa Rais Ruto wazua gumzo Kenya
KimataifaTangulizi

Mshahara wa milioni 28 kwa Rais Ruto wazua gumzo Kenya

Spread the love

RAIS wa Kenya, William Ruto, naibu wake Rigathi Gachagua na Katibu Mkuu Mkuu, Musalia Mudavadi kuwa ni moja ya maafisa wa ngazi ya juu serikali ya nchi hiyo wanaoongoza kwa mishahara mikubwa katika nyongeza ya mishahara iliyopendekezwa hivi karibuni. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Tume ya Mishahara ya nchi hiyo (SRC) ilichapisha mapendekezo hayo kwenye kalenda yake kwa mwaka wa kifedha 2023/2024.

Kwa mujibu wa pendekezo la mishahara, maafisa wa serikali watasubiriwa ongezeko la asilimia 14 kuanzia tarehe 1 Julai 2023.

Aidha, kutokana na taarifa hiyo, tayari mjadala umeanza kushika kasi katika mitandao ya kijamii hasa ikizingatiwa serikali hiyo imekuwa ikilia kuwa na ukata wa fedha.

Baada ya kuchukua hatamu za uongozi, Naibu rais Rigathi Gachagua alisema walihidi kupunguza makali ya maisha kwa wananchi kwa kupunguza baadhi ya gharama zisizo za lazima Serikali.

Bloga maarufu nchini humo Pauline Njoroge ni miongoni mwa wale ambao wameanza kuikosoa serikali akisema Kenya Kwanza wameharibu uchumi na sasa wanataka kula zaidi.

Ikiwa pendekezo litapitishwa, Rais atapokea KSh 1.65 milioni (TSh. 28.3 milioni) kuanzia Julai 1, 2024.

Naibu Rais atapata KSh 1,367,438 (Tsh. 23.4 milioni), kutoka KSh 1,227,188 (Tsh 21 milioni) na ongezeko lingine hadi KSh 1.4 milioni (Tsh. 24 milioni) Julai 1, 2024, ambayo ni ongezeko la 14%.

Katibu Mkuu Mkuu Musalia Mudavadi na mawaziri wengine watapokea KSh 1,056,000, kutoka KSh 924,000, kuanzia Julai 1, 2023.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

error: Content is protected !!