Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mahakama yabatilisha uamuzi wa Baraza Kuu Chadema kesi ya akina Mdee
Habari za SiasaTangulizi

Mahakama yabatilisha uamuzi wa Baraza Kuu Chadema kesi ya akina Mdee

Spread the love

MAHAKAMA Kuu Tanzania  Masjala ya Dar es Salaam imebatilisha uamuzi wa Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) lililobariki uamuzi wa Kamati Kui Chadema kuwavua uanachama akina Halima Mdee na wenzeka 18. Anaripori Faki Sosi…(endelea).

Uamuzi huo umetolewa leo tarehe 14 Desemba na Jaji Cyprian Mkeha ambapo amesema kuwa Baraza kuu la chama hicho halikutoa haki ya asili kwa waombaji (Mdee na wenzake.

Kuhusu hoja ya waleta maombi kudai hawakupewa muda wa siku 14 kujitetea, Mahakama imebainisha kuwa walipewa nafasi ya kusikiliza na hawakuitumia.


Amedai Kamati Kuu ya Chadema iliyoketi Novemba 2020 kwa mujibu wa Katiba ya Chadema walikua na mamlaka ya kusikiliza shauri lao kwa njia ya dharura, na taratibu zote ambazo walistahili kuzizingatia zilizingatiwa.

Aidha, amedai uamuzi wa Baraza Kuu wa kusikiliza rufaa za Mdee na wenzake uliofanywa Mei mwaka jana na baadhi ya wajumbe walioshiriki kutoa uamuzi ndani ya Kamati Kuu, halikuwa jambo si sahihi kwa mujibu wa taratibu.

“Ilionekana wajume 23 wa Kamati Kuu  walioshiriki akiwemo Mwenyekiti na Katibu Mkuu walishiriki kupiga kura kwenye Baraza Kuu la Chadema jambo ambalo sio sahihi.

“Kwa hilo nikasema ni kweli kanuni hiyo ya haki ya asili inayomzua mtu kuwa muamuzi katika shauri lake mwenyewe imekiukwa na haijapingwa” amesema Mkeha

Jaji Mkeha amesema kuwa maombi hayo hayakubishaniwa juu ya kuwa na vigezo ama lah!

Katika hukumu hiyo Jaji Mkeha ameeleza kuwa hajafuta uamuzi uliotolewa na Kamatu Kuu ya Chadema.

“Sijafuta uamuzi wa Kamati Kuu, Uamuzi ambao nimeufuta ni ule wa Baraza  Kuu kwa kuwa watu walioshiriki ni wale wale”

Jaji Mkeha ameiagiza  Chadema izingatie kanuni asilia za haki itakapotakiwa kuamua haki ya rufaa ya watoa maombi.

Mdee na wenzake 18 walienda mahakamani kupinga uamuzi wa Baraza Kuu Chadema lililoketi Mei mwaka jana kubariki uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho ambao uliwafuta uanachama makada hao.

Mdee na wenzake 18 walituhumiwa kwenda bungeni kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalumu Chadema bila ridhaa ya chama hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!