March 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mahakama Kenya yazidi kuanika madudu ya Tume

Naibu Jaji Mkuu wa Kenya Philomena Mwilu

Spread the love

NAIBU Jaji Mkuu wa Kenya Philomena Mwilu, amesema kitendo cha Tume ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC), kushindwa kufuata maagizo ya mahakama ya juu nchini humo,  kinadhihirisha kuwa madai ya udukuzi yaliyotolewa na upinzani yalikuwa ya ukweli, anaandika Mwandishi wetu.

Jaji Mwilu amesema mahakama ilikubaliana na madai ya upinzani kuwa matokeo yalitangazwa kabla ya matokeo yote kutoka kwa vituo 40,000 kupokelewa.

“Uchaguzi haukuwa na uwazi na hatukuwa na lingine ila kuufuta,” Jaji amesema

Jaji Mwilu amesema IEBC ilitegemea ripoti za waangalizi wa uchaguzi kuamua kuwa uchaguzi ulikuwa wa haki na siyo vinginevyo.

Waangalizi walikosolewa vikali wakati uchaguzi ulipofutwa baada ya kutangaza harakaharaka kwamba ulikuwa huru na wenye uwazi.

Kwa upande wake Jaji Mkuu nchini Kenya, David Maraga, amesema kuwa upinzani hakubaini madai yao kwamba kampeni za rais zilitumia fedha za umma.

Jaji Maraga amesema kuwa sampuli kadha za fomu zilionyesha kuwa hazikuwa na mihuri rasmi, zingine hazikwa na sahihi na namba za usajili wala alama rasmi.

Amesema kuwa uchaguzi haukufutwa tu kwa sababu ulikuwa na hitilafu, lakini ulifutwa kwa sababu hitalafu hizo zilishawishi matokeo.

Baada ya Mahakama ya juu kufuta matokeo hayo, kumeibuka mabishano ya kisiasa kati ya Muungano wa Nassa chini ya Raila Odinga na Jubilee ambao wanaongoza serikali chini ya  Rais Uhuru Kenyatta.

error: Content is protected !!