SERIKALI ya Tanzania imetoa tathmini ya athari ya mafuriko yanayosababishwa na mvua kubwa inayonyesha mfululizo katika baadhi ya mikoa nchini, ikisema yameua watu 28 mkoani Morogoro na watano Pwani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).
Ripoti ya athari ya mafuriko imetolewa leo Ijumaa, tarehe 12 Aprili 2024, jijini Dar es Salaam na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi, huku Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), ikitoa tahadhari ya uwepo wa mvua kubwa katika mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Morogoro, Pwani, Lindi na Mtwara, kati ya tarehe 12 hadi 14 Aprili mwaka huu.
Matinyi amesema mafuriko hayo pamoja na kusababisha vifo, imeleta maafa katika halmashauri nane za Morogoro ambapo nyumba zaidi ya 6,800 zikizingirwa maji na kubomoa 1,035.
“Morogoro kuna vifo 28 na Pwani kuna vifo vya watu watano, watu wawili wamefariki wilayani Rufiji na wawili Kibiti na mmoja Kisarawe. Majeruhi wawili wilayani Kibiti na majeruhi watatu Kisarawe. Makazi ya barabara, makazi, madaraja nguzo ya umeme, shule na kituo cha afya mhoro Rufiji kimesomwa na maji, lakini kuna uharibifu wa mazao mengi ya chakula mahindi, mpunga, ufuta, ndizi mihogo na mtama,” amesema Matinyi.
Leave a comment