Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wanafunzi 7 wahofiwa kufariki gari la shule likitumbukia korongoni
Habari Mchanganyiko

Wanafunzi 7 wahofiwa kufariki gari la shule likitumbukia korongoni

Spread the love

 

WANAFUNZI saba wanahofiwa kupoteza maisha, huku watatu wakinusurika katika ajali ya gari la shule ya msingi Ghati Memorial, lililotumbukia katika korongo lililopo maeneo ya mitaa ya Dampo, Kata ya Sinoni jijini Arusha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Tukio hilo limetokea asubuhi ya leo tarehe 12 Aprili 2024, huku chanzo kikidaiwa ni uzembe wa dereva kwa kutaka kulazimisha kupita sehemu ambayo maji ya mafuriko ya mvua yanapita kwa kasi, kitendo kilichopelekea gari kusombwa na kutupa korongoni ambalo linapitisha maji.

Inadaiwa kuwa, gari hilo lilikuwa limetoka kuwachukua wanafunzi majumbani mwao kisha kuwapeleka shule maeneo ya Engesengiu.

Kamanda wa Polisi Arusha, SACP Justine Masejo, amesema kikosi cha uokoaji kipo eneo la tukio kwa ajili ya kuwafutilia wanafunzi saba ambao hawajulikani walipo, kisha atatoa taarifa kamili baadae.

“Nipo kwenye msafara, ila hizo taarifa nimezipata, kikosi cha Uokozi kipo eneo la tukio na Wanafunzi saba hawajulikani walipo wengine wameokolewa, taarifa kamili tutaitoa baadaye,” amesema Kamanda Masejo.

Akizungumza na waandishi wa habari akiwa eneo la tukio, Diwani wa Kata ya Sinoni, Michael Kivuyo, amesema wananchi kwa kushirikiana na kikosi cha uokoaji wanashirikiana katika zoezi la kuwatafuta wanafunzi saba waliopotea.

Kwa mujibu wa kivuyo, gari hilo lilikuwa na watu 13 wakiwemo wanafunzi 11, dereva na matroni.

“Waliokuwa kwenye gari ni wanafunzi 11, akiwemo dereva na matroni. Kati yao hao 11 wanafunzi Watatu, dereva na matroni wameokolewa, mwili mmoja umepatikana, Wananchi wameingia mtoni, wengine wamepewa usafiri kufuata uelekeo wa mto ili kuwatafuta ambao hawajapatikana,” amesema Kivuyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!