Saturday , 4 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Maaskofu Katoliki wapata ajali Chato
Habari Mchanganyiko

Maaskofu Katoliki wapata ajali Chato

Askofu Severine Niwemugizi, Jimbo Katoliki la Rulenge-Ngara
Spread the love

 

MAASKOFU wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania, Paul Ruzoka wa Jimbo Kuu la Tabora na Severin Niwemugizi wa Jimbo la Rulenge-Ngara mkoani Kagera, wamepata ajali gari eneo la Buziku, wilayani Chato mkoa wa Geita. Anaripoti Mwandishi Wetu, Chato … (endelea).

Ajali hiyo imetokea mchana wa leo Alhamisi, tarehe 4 Novemba 2021, wakati maaskofu hao wakitoka kikaoni Mwanza, kwenga Ngara katika msiba wa Padre wa Jimbo hilo aliyefariki dunia jana Jumatano.

Akizungumza na MwanaHALISI Online kwa simu, Askofu wa Jimbo la Geita, Fravian amesema, maaskofu hao walikuwa katika kikao cha kamati tendaji cha Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Igombe jijini Mwanza.

Amesema, jana Jumatano kuna Padre wa Jimbo la Rulenge-Ngara alifariki dunia katika Hospitali ya Bugando, Mwanza hivyo kulazimka kwenda msibani na Askofu Ruzoka akamsindikiza.

“Ni kweli ajali imetokea kabla ya saa 6 mchana, baada ya kutokea kwa msiba wa Padre wa Jimbo hilo, wameondoka asubuhi na wakiwa wamepita eneo la Buziku kuna mtu aliingia barabarani ghafla.

“Katika jitihada za kumkwepa yule mtu akarudi ule upande waliokuwa wamemkwepea, ili wasimdhulu ikabidi amkwepe tena upande wa pili na ndipo gari ilipoanguka,” amesema Askofu Kasala

Amesema “kwa bahati yule mtu hakudhulika na maaskofu wametoka salama na wameumia kidogo.”

Askofu Kasala amesema, “baada ya ajali hiyo wamepelekwa Parokoa ya Buziku na baadaye wamepelekwa Hospitali ya Biharamulo kwa ajili ya uchunguzi ili kuona hali zao kabla ya kuendelea na safari.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

error: Content is protected !!