Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mwigulu ataja mabilionea 5000 wa Tanzania, Msukuma yumo
Habari za Siasa

Mwigulu ataja mabilionea 5000 wa Tanzania, Msukuma yumo

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango
Spread the love

 

WAZIRI wa Fedha na Uchumi, Dk. Mwigulu Nchemba amesema Tanzania ina jumla ya mabilionea 5,740 sawa na asilimia 4.2 ya utajiri katika kundi la mabilionea 140,000 waliopo Barani Afrika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Dk. Mwigulu ametoa kauli hiyo leo tarehe 4 Novemba, 2021 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Mlalo, Rashid Abdallah Shangazi (CCM).

Shangazi amehoji Tanzania ina idadi ya watu takribani milioni 55 wenye madaraja tofauti ya uchumi; Je, katika idadi hiyo Tanzania ina mabilionea wangapi?

Akijibu swali hilo, Nchemba amesema kutokana na utafiti uliofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mwaka 2014/2015 na kurejewa mwaka 2019/2020, unaonesha idadi ya mabilionea duniani inakadiriwa kufikia watu milioni 14.

“Na kwa mujibu wa ya report ya RBC Wealth management ya Julai mwaka 2019, bara la Afrika lina mabilionea 140,000 sawa na asilimia moja ya mabilionea wote duniani,” amesema.

Amesema miongoni mwa mabilionea 5,740, waliopo Tanzania, mabilionea 115 sawa na asilimia mbili ya utajiri wa dola za Marekani milioni 30, wanamiliki zaidi ya asilimia 28 ya utajiri wote wa mabilionea wanaotoka Tanzania.

“Kati ya hawa wengi wamesajiliwa TRA, na wanalipa kodi zao katika idara ya walipa kodi wakubwa. Na wamewekeza katika sekta ya viwanda, nishati, madini na wamewekza pia katika sekta ya fedha, mawasiliano, uchukuzi, utalii na makazi,” amesema.

Aidha, amesema mabionea hao wanatoka katika sekta mbalimbali kama vile madini, viwanda, mawasiliano na ujenzi na sekta nyingine ambazo hakuzitaja lakini na wenyewe wapo kama akina King Msukuma.

3 Comments

  • Mabilionea wa Ulaya wametajirika kutikana na madini yetu. Tuambie, kati ya hao mabilionea wa next, ni wangapi wanatJirika kutokana na madini yetu..
    Anzia na wamiliki wa Williamson Diamond 💎, African Barrick Gold na wengineo.
    Pia, ni lini Idara ya Kodi ya Mapato na Ile Idara ya Ushuru wa Forodha zikatenganishwa? Fedha nyingi hazilipwi kwa sababu ushuru wa forodha haipo Tena. TRA ni kubwa meno ndiyo maana mafuta na vitu vingine vinapitishwa bandaging Bill kulipiwa.

  • Mabilionea wa Ulaya wametajirika kutokana na madini yetu. Tuambie, kati ya hao mabilionea wa nje, ni wangapi wanatajirika kutokana na madini yetu..
    Anzia na wamiliki wa Williamson Diamond 💎, African Barrick Gold na wengineo.
    Pia, ni lini Idara ya Kodi ya Mapato na Ile Idara ya Ushuru wa Forodha zikatenganishwa?
    Fedha nyingi hazilipwi kwa sababu Idara ya Ushuru wa Forodha haipo Tena. TRA ni kubwa mno ndiyo maana mafuta na vitu vingine vinapitishwa kinyemela bila kulipiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!