Monday , 4 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lowassa afariki dunia, magonjwa 3 yatajwa
Habari za SiasaTangulizi

Lowassa afariki dunia, magonjwa 3 yatajwa

Spread the love

Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Edward Lowassa (70) amefariki Dunia leo tarehe 10 Februari 2024 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini (JKCI) Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akitangaza kifo hicho kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia televisheni ya Taifa (TBC), Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango amesema Lowassa amefariki leo saa nane mchana.

Amesema Lowassa amefariki katika hospitali hiyo ya JKCI alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa kujikunja utumbo, matatizo ya mapafu na shinikizo la  damu.

“Lowassa ameugua kwa muda mrefu, amekuwa akipatiwa matibabu tangu tarehe 14 Januari 2022 katika hospitali ya JKCI na baadae Afrika kusini na kurejea JKCI.

“Rais Samia aanatoa polea kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huu mkubwa pia ametangaza siku tano za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa,” amesema Dk. Mpango.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwinyi aungana na Samia kuuaga mwili wa baba yake

Spread the loveRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mtoto wa Mzee Mwinyi amwaga machozi

Spread the loveMtoto wa Hayati mzee Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi ameshindwa...

Habari za SiasaTangulizi

Mzee mwinyi alikuwa mwanademokrasia wa kweli

Spread the loveMtoto wa Hayati Ali Hassan Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Mwinyi alikuwa maktaba inayotembea

Spread the loveRais Samia Suluhu hassan amesema Hayati rais mstaafu, Ali Hassan...

error: Content is protected !!