Monday , 4 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79 ikiwamo TZ
Kimataifa

Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79 ikiwamo TZ

Rais Lazarus Chakwera
Spread the love

Waziri wa usalama wa ndani nchini Malawi, Ken Zikhałe ametangaza mabadiliko ya kanuni za uhamiaji nchini humo kwa kuondoa vizuizi vya viza kwa raia kutoka Uingereza, China, Urusi, Ujerumani, Australia, Canada, Ubelgiji, Ghana, Gambia, Sierra Leone, Ufaransa na nchi nyengine.

Pia raia kutoka nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (Sadc) ikiwamo Tanzania na soko la pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (Comesa) pia wameondolewa vikwazo hivyo vya viza. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Amesema hatua hiyo ya serikali haijumuishi nchi zinazowataka raia wa Malawi kuwa viza wakati wakizuru mataifa hayo.

Ubalozi wa Uingereza nchini Malawi uliwataka raia wake kuchukua fursa hiyo ya serikali kutembelea vivutio vingi vya utalii katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.

Malawi inaungana na Kenya na Rwanda kufungua nchi zao kwa wasafiri kutoka barani Afrika bila vikwazo vya visa.

Nchi hizo mbili za Afrika Mashariki zimetangaza kuingia bila viza kwa wageni kutoka bara Afrika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wanajeshi Ukraine waishiwa risasi, 31,000 wauawa

Spread the loveRais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema zaidi ya wanajeshi 31,000...

Kimataifa

Waziri mkuu Palestina ajiuzulu

Spread the loveWaziri Mkuu wa Palestina, Mohammed Shtayyeh ametangaza kujiuzulu pamoja na...

Kimataifa

Rais mstaafu ahukumiwa miaka 4 jela

Spread the loveMahakama ya mjini Tunis imemhukumu rais wa zamani wa Tunisia,...

Kimataifa

Jeshi Kongo lazima jaribio la M23

Spread the loveJeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo jana Jumatano lilizima...

error: Content is protected !!