Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu atoa msimamo, kamati kuu Chadema yaitwa
Habari za Siasa

Lissu atoa msimamo, kamati kuu Chadema yaitwa

Spread the love

TUNDU Antiphas Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amesema, uamuzi uliofanywa na Kamati ya Maadili ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wa kumsimamisha kufanya kampeni siku saba haukuzingatia utaratibu wa kisheria na kanuni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea)

Amesema, amehukumiwa bila kupewa tuhuma kwa maandishi, kuwasilisha utetezi wake na kusikilizwa kama Kanuni za Maadili ya Uchaguzi ya Urais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2020 zilizotolewa na NEC zinavyoelekeza.

Uamuzi wa kamati ya maadili umetolewa leo Ijumaa tarehe 2 Oktoba 2020 na Emmanuel Kawishe, Katibu wa kamati hiyo ukionyeshwa Lissu amesimamishwa kufanya kampeni kwa siku saba kuanzia kesho Jumamosi hadi 9 Oktoba 2020.

Kawishe amesema, Lissu amekutana na kadhia hiyo baada ya malalamiko yaliyowasilishwa na chama cha NRA na Chama Cha Mapinduzi (CCM) vikimtuhumu kutoa mameno ya uchochezi yasiyothibitika.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Tegeta jijini Dar es Salaam leo Ijumaa , Lissu amesema “hadi sasa (ilikuwa saa 11 jioni) sijapewa malalamiko yoyote ya maandishi ya hivyo vyama NRA na CCM kinyume cha kanuni za maadili ya uchaguzi.”

“Hadi sasa, sijapewa fursa ya kuwasilisha utetezi wa maandishi dhidi ya ukiukwaji wa maadili niliyoambiwa nimeyafanya na hakuna wito wowote nimeletewa kuhudhuria kikao cha kamati ya maadili,” amesema Lissu

Amesema, kutokana na uamuzi huo, Kamati Kuu ya Chadema “inakutana kesho katika kikao cha dharula kujadili suala hili na kutoa uamuzi, lakini msimamo wangu binafsi, kampeni zangu zinaendelea Jumapili kama ilivyopangwa kwenye ratiba ya tume.”

“Kama kamati kuu itasema subiri siku saba ziishe nitasubiri lakini kwa vile haijasema mimi naendelea na maandalizi ya kampeni,” amesema Lissu

Kwa mujibu wa ratiba ya kampeni, inaonyesha Jumapili ya tarehe 4 Oktoba 2020 ataendelea na kampeni baada ya kupumzika kwa siku tatu na atakuwa Mkoa wa Pwani katika Majimbo ya Kibaha na Kisarawe.

Tarehe 5 Oktoba 2020, ratiba inaonyesha atakuwa na mikutano mkoani huko kwenye majimbo ya Kibiti na mkuranga.

Katika mkutano wake huo na waandishi, Lissu amesema, kila mgombea wa urais, ubunge na udiwani walisaini maadili ya uchaguzi na wanapokosea au lolote wanapaswa kuwasiliana naye moja kwa moja kwa mambo waliyofanya wagombea na kama ni chama basi malalamiklo yanapelekwa kwenye chama.

Amesema, barua ya malalamiko ilipelekwa makao makuu ya Chadema kinyume na kanuni hizo za maadili kwani tume ilikuwa na uwezo wa kujua yuko wapi ili wamfikishie moja kwa moja.

“Natembea na askari polisi nyuma ya kiti cha gari kila ninapokwenda, katika msafara wangu kuna magari mawili ya polisi nyuma na mbele na ninapo lala kuna askari wanalinda na tume ina ratiba ya kampeni inayoweza kuwasaidia niko wapi ili wanifikishie mimi malalamiko hayo.”

“Uamuzi huu si wa haki, kwani haki inadai mtuhumiwa apewe tuhuma zake kabla hajaadhibiwa na ni kinyume cha sheria kumuadhibu mtu bila kumsikiliza na uamuzi huu haukubaliki kwa namna yoyote ile,” amesema Lissu ambaye kitaaluma ni mwanasheria

Lissu amesema, kwa nyakati tofauti tangu tarehe 21 Septemba 2020, “sisi Chadema, tumepeleka malalamiko matatu tume dhidi ya mgombea wa CCM, Rais John Magufuli yanayohusu rushwa ya uchaguzi, kutoa ahadi za maendeleo kinyume na kuni za uchaguzi, niambieni kama mmesikia tume ikizungumzia malalamiko yetu na malalamiko kama haya haya tumeyapeleka ofisi ya msajili lakini wote wako kimya.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Spika Tulia aibana Serikali mafao ya wastaafu Jumuiya ya Afrika Mashariki

Spread the loveSPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameitaka Serikali kufanya tathimini...

Habari za Siasa

Serikali yawapa maagizo Ma-RC udhibiti magonjwa yasiyoambukiza

Spread the loveWAKUU wa mikoa nchini wametakiwa kuandaa utaratibu wa kuwawezesha wananchi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

error: Content is protected !!