Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Treni ya abiria Dar-Arusha yazinduliwa
Habari Mchanganyiko

Treni ya abiria Dar-Arusha yazinduliwa

Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC),Aboubakar Kunenge amezindua safari ya kwanza ya treni ya abiria kutoka Dar es salaam kwenda Mkoani Arusha. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Usafiri huo uliokuwa umekosekana kwa takribani miaka 30 na kusababisha adha ya usafiri kwa wananchi umezinduliwa leo Ijumaa tarehe 2 Oktoba 2020 jinini Dar es Salaam.

Akizindua safari hiyo, Kunenge amelielekeza Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora za usafiri na kuwapongeza kwa mapinduzi wanayoyafanya kwenye usafiri wa Reli.

Aidha, Kunenge amesema, treni hiyo itasaidia wafanyabiashara na wananchi hususani wa kipato cha kawaida kupata usafiri wa haraka na kwa bei nafuu hivyo ametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa hiyo.

Kunenge ameipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John pombe Magufuli kwa kutekeleza kwa vitendo ahadi alizotoa na maamuzi yake ya kufufua usafiri wa treni.

Kwa upande wake, Mkurugwnzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema shirika hilo limejidhatiti vyema kuhakikisha linatoa huduma bora na salama kwa wananchi wote.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!