Monday , 27 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa lMajaliwa: Hatuwezi kuwaacha wasanii
Habari za Siasa

lMajaliwa: Hatuwezi kuwaacha wasanii

Spread the love

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amesema, Serikali ijayo ya chama hicho itaendelea kuwaunga mkono na kuwaendeleza wajasiriamali wakiwemo wasanii. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

“Serikali ya CCM inawathamini sana wasanii kwa sababu sanaa ni sawa na ujasiriamali. Kwa maana hiyo, sanaa ni ajira,” alisema Majaliwa

Ametoa kauli hiyo jana jioni Ijumaa tarehe 2 Oktoba 2020 wakati akizungumza na wakazi wa wilaya ya Kahama katika mkutano uliofanyika uwanja wa Magufuli mjini Kahama, mkoani Shinyanga.

Akielezea kuhusu ujenzi wa barabara za kuunganisha mikoa, Majaliwa alisema kwenye ilani ya uchaguzi, barabara kubwa inayotajwa kuunganisha mji wa Kahama na mikoa ya jirani ni ya kutoka Katavi hadi Tabora kupitia Ugalla.

“Katika uk. 73, Ilani yetu inataja barabara zinatotakiwa kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami ambazo ni Mpanda – Ugala – Kaliua – Ulyankulu – Kahama (km 428); Geita – Bukoli – Kahama (km 107) na Kahama – Nyamilangano – Uyogo (km 54).”

Majaliwa ambaye amemaliza ziara yake ya kumuombea kura mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, John Pombe Magufuli alimnadi pia mgombea ubunge wa Kahama Mjini, Jumanne Kishimba na wagombea udiwani wa wilaya hiyo.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Madini, Dotto Biteko alisema wilaya ya Kahama imepanda chati ya makusanyo yatokanayo na madini kutokana na usimamizi wa Serikali ya awamu ya tano.

“Kwenye makusanyo ya madini, Kahama ilikuwa ikishika nafasi ya nne. Sasa hivi imepanda na kuchukua nafasi ya pili. Mnashindana na Geita. Chunya ndiyo ilikuwa ikishika nafasi ya pili, lakini sasa hivi mmeiacha mbali. Chagueni viongozi wa CCM ili iendelee kuwaletea neema,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kasekenya aipa Tanroads wiki kukarabati barabara Morogoro

Spread the loveNaibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja...

Habari za SiasaTangulizi

‘Aliyemtonya’ Lissu kuhusu rushwa arejea madarakani

Spread the loveMwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Iringa, William Mungai...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Tutaendelea kupigania malengo ya afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema dhamira ya Tanzania...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NHC yadai bil. 2.1 taasisi za Serikali, Waziri atoa maagizo

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii...

error: Content is protected !!