Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu aibuka mkutano wa Chadema, atoa hutuba nzito kwa wajumbe
Habari za Siasa

Lissu aibuka mkutano wa Chadema, atoa hutuba nzito kwa wajumbe

Spread the love

TUNDU Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Mandeleo (Chadema) ameibuka katika mkutano Mkuu wa chama hicho leo na kuzungumza na wajumbe wa mkutano huo. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza kwa njia ya video kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp leo tarehe 18 Desemba 2019, Lissu amesema chama hicho kwa sasa kina nguvu zaidi kuliko juzi na jana.

“Baada ya mateso na uhuni wote tuliofanyiwa, njia iliyobaki sasa ni kuchukua nchi mwaka ujao, wametupa mateso ya kila aina lakini leo tuna nguvu zaidi kuliko iliyokuwa juzi na jana,” amesema. 

Lissu ambaye pia ni Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti katika uchaguzi wa viongozi wakuu wa chama, ameleeza wajumbe wa mkutano pamoja na kujeruhiwa, kufungwa kwa baadhi ya wafuasi wa chama hicho lakini wasiache kufanya maandalizi ya kutosha ya kuirejesha nchi kwenye demokrasia na haki.

Lissu amewataka viongozi na wafuasi wa Chadema kuandaa mazingira yenye usalama ili arejee nchini.

“Nimepona na nipo tayari kurudi nyumbani, kuja kuungana na makamanda na watanzania ili tutengeneze nchi mpya yenye kujali utu, mfanye linalowezekana ili nirudi nyumbani katika mazingira ya usalama,” amesema Lissu.

Wakati Lissu anazungumza na wajumbe wa Mkutano huo wafuasi waliokuwepo kwenye ukumbi wa mikutano wa Mlimani City walisimama na kumshangilia kwa sauti ya juu wakisema ‘People’s Power’

Wakati wote Lissu amezungumza kwa hisia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!