Sunday , 5 February 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Kutimuliwa viongozi DARUSO: Wanasiasa, wanaharakati wamvaa Prof. Ndalichako
ElimuHabari Mchanganyiko

Kutimuliwa viongozi DARUSO: Wanasiasa, wanaharakati wamvaa Prof. Ndalichako

Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu
Spread the love

BAADHI ya Wanasiasa na Wanaharakati wamepinga utekelezwaji wa agizo la Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu,  la kuwachukulia hatua viongozi wa Serikali ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO), walioshinikiza changamoto za mikopo, kutatuliwa ndani ya saa 72. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Jana tarehe 17 Desemba 2019 Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kupitia Prof. William Anangisye, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, ulitekeleza agizo la Prof. Ndalichako kwa  kuaandika barua ya kuwasimamisha masomo, viongozi sita wa DARUSO, kwa tuhuma za kukiuka sheria za chuo hicho.

Kwa mujibu wa barua hiyo, wanafunzi hao wa UDSM wanatuhumiwa kuanzisha harakati, zinazohatarisha amani na usalama katika mazingira ya usomaji chuoni hapo. Sambamba na kuhamasisha wanafunzi wengine kushiriki uasi huo.

Kufuatia hatua hiyo, wanasiasa na wanaharakati wamesema hatua hiyo sio suluhisho, katika kutatua changamoto zilizolalamikiwa na DARUSO.

Bonifacia Mapunda, Mwenyekiti Ngome ya vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, amesema hatua hiyo inakiuka haki za msingi za wanafunzi hao.

“Kitendo cha Waziri wa Elimu DR. Ndalichako kuagiza viongozi wa wanafunzi hao kuchukuliwa hatua kali, si suluhisho la kutatua changamoto zilizopo vyuoni na kinatia hofu zaidi,” inaeleza taarifa ya Mapunda.

Ngome hiyo imeutaka uongozi wa UDSM kuwarudisha chuoni bila masharti, viongozi hao wa DARUSO.

“Wanafunzi waliosimamishwa waachiwe haraka na bila masharti. Serikali ipeleke pesa Bodi ya Mikopo na iwaagize Bodi kuwalipa pesa wanafunzi hao kwa haraka,” inaeleza taarifa ya Mapunda na kuongeza;

“Rais atimize ahadi yake aliyoitoa kipindi cha kampeni kuwa mwanafunzi akicheleweshewa mkopo wake, aliyefanya hivyo atafukuzwa haraka. Prof. Ndalichako awajibike  kwa kushindwa kutatua tatizo hili kwa muda mrefu na kuchochea vurugu zaidi.”

Fatma Karume, aliyekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), amelaani hatua hiyo, na kutoa wito kwa wanafunzi wa UDSM kupaza sauti zao, ili wanafunzi hao warudishwe masomoni.

Mwanaharakati Shamira Mshangama, amesema wanafunzi hao wameonewa kwa kutuhumiwa kufanya uasi, kwa madai kwamba, walichukua hatua hiyo ili kutuliza ghasia.

“Mamlaka zinajuaje labda Viongozi hawa walitumia njia ya Bandiko kwa lengo la kutuliza maandamano? Wanafunzi wamekaa miezi miwili bila pesa zao, leo viongozi wanadai wanasimamishwa masomo, badala ya kupewa maneno ya kuwafariji na kuwaelekeza walipokosea,” ameandika Mshangaka katika ukurasa wake wa Twitter.

Naye Abdul Nondo ameandika “Yaani viongozi hawa wamesimamishwa chuo kusubiri hatua za kinidhamu , katika hatua za kinidhamu ndio wataitwa kusikilizwa . Yaani wanafunzi wanasimamishwa kwa muda usio fahamika alafu ndio wataitwa kusikilizwa kwa muda usio fahamika.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awalilia 17 waliofariki ajalini wakisafirisha maiti

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa...

Habari Mchanganyiko

Wanawake wachimbaji wajenga zahanati kuokoa afya za wakazi 2000

Spread the love  ZAIDI wakazi 2,000 wa kijiji cha Nyamishiga Kata ya...

Habari Mchanganyiko

Baada ya Congo DR, Somalia mbioni kujiunga na EAC

Spread the love  TAIFA la Somalia liko mbioni kuwa mwanachama rasmi wa...

error: Content is protected !!