April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

JPM akerwa na mlundikano wa mahabusu, atoa agizo

Rais John Magufuli

Spread the love

RAIS John Magufuli amesema ni aibu nchi kuwa na idadi kubwa ya mahabusu, kuliko wafungwa. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 18 Desemba 2019, wakati akifungua jengo la Mahakama ya Wilaya ya Chato, mkoani Geita.

“Ni aibu kuwa na idadi kubwa ya mahabusu kuliko idadi ya wafungwa. Mnaweza mkaona changamoto tuliyonayo ya kupunguza mahabusu,” ameeleza Rais Magufuli.

Kufuatia changamoto hiyo, Rais Magufuli ameagiza vyombo vya dola kushirikiana na mahakama ili kuitatua changamoto hiyo.

Rais Magufuli amevitaka vyombo vinavyotoa haki kuimarisha mfumo wa utoaji haki ili kuharakisha uendeshaji wa mashtaka.

“Nitoe agizo kwa¬†Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), ofisi ya DPP, wakili mkuu wa serikali na polisi kushirikiana na mahakama ili kuimarisha mfumo wa haki na kuharakisha uendeshaji mashtaka nchini,” ameagiza Rais Magufuli.

error: Content is protected !!