September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lwaitama atupa dongo kwa Sumaye

DK. Azaveli Lwaitama, Mhadhiri mstaafu

Spread the love

DK. Azaveli Lwaitama, Mhadhiri mstaafu, ameutumia Mkutano Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutupa jiwe gizani kwa serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Hamis Mguta…(endelea).

Lwaitama ambaye ni Mwanachama hai wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ametumia nafasi hiyo leo tarehe 18 Desemba 2019 katika mkutano huo ambao utafanya uchaguzi wa mwenyekiti wa chama na Makamu Mwenyekiti wa chama Taifa usiku huu.

Amesema kuwa maendeleo bila demokrasia yanaweza yakawa yananufaisha watu wachache na wakati mwingine vipaumbele vya nchi vinatengenezwa na watu wachache.

“Mtu anaweza kutembea na hela yake anapita mitaani anagawa, anaweza kuamua leo tutajenga lakini mikopo kwa wanafunzi tutachelewesha.

“Tungekuwa na Bunge linalokaa na kujadili labda tungebishana, wakati mwingine kukosekana kwa demokrasia kunaweza kubadilisha vipaumbele vya maendeleo,…sizungumzi juu ya mtu nazungumzia umuhimu wa demokrasia,” amesema Lwaitama bila kumtaja anayemlenga.

Wakati Lwaitama akiyasema hayo, kumekuwa na malalamiko mbalimbali kutoka kwa vyama pinzani vya siasa nchini vikidai kuwa serikali ya CCM imeminya demokrasia kwa kusitisha bunge kurushwa mubashara na hata kulalamika ya kuwa rais Magufuli anafanya maendeleo ya vitu na sio ya watu kwa kununua ndege na kujenga miundombinu ya barabara huku wananchi wakiwa na maisha magumu.

https://youtu.be/uNz5UBWh3Qg

Ameenda mbali zaidi na kugusia juu ya uwepo wa demokrasia ndani ya Chama cha Chadema, na kusema kuwa chama tawala hakina utaratibu wa kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama kama ilivyo ndani ya Chadema hivyo Chadema ina demokrasia kuliko CCM.

“Demokrasia ilivyo nzuri hata kama mna kiongozi ambaye mnamkubali mnamruhusu mtu mwingine ashindane naye lakini kile chama kingine watu wanahojiwa kwa kufikiria tu namimi nigombee, kuna ndugu yangu mmoja alikuja kwetu na baadaye akaenda kuanzisha chama kingine kule alikokuwa mwanzoni walimzuia asigombee,” amesema.

Amesema kuwa katika chama cha Chadema hakuna kitu kupita bila kupingwa kwa mgombea wa nafasi yoyote bali hata kama ukiwa unagombea peke yako unapigiwa kura za ndio au hapana, wengine wakipigiwa kura ya hapana inakuwa nongwa wanarudi kwao.

error: Content is protected !!