Thursday , 13 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kubenea amjia juu Mwigulu
Habari za SiasaTangulizi

Kubenea amjia juu Mwigulu

Saed Kubenea, Mbunge wa Ubunge akizungumza na waandishi wa habari. Picha ndogo, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani
Spread the love

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Lameck Nchemba, kujiuzulu mara moja wadhifa wake. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari mchana wa leo Jumatano, jijini Dar es Salaam, Kubenea amesema, Mwigulu anapaswa kujiuzulu, kufuatia jeshi la polisi, kutuhumiwa kumminia kwa risasi, Akwilina Akwilini, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza kutoka Chuo cha Usafirishaji (NIT).

Anasema, “naungana na wanafunzi wa NIT na wale wa vyuo vikuu vingine nchini; mashirika ya madhehebu ya kidini, vyama vya hiari, asasi za kiraia na wote wanaolitakia mema taifa hili, kumtaka mheshimiwa Mwigulu Nchemba, kujiuzulu mara moja kufuatia kifo hiki cha Akwilina.”

Amesema, “…utetezi wake kuwa mauaji yale yamefanywa na Chadema, hauna mashiko. Ni utetezi uliosheheni matundu na hivyo hauwezi kukubalika kwenye sura za wananchi. Ni vema akajiuzulu ili kulinda heshima yake.”

Akwilina alipigwa risasi kichwani, Ijumaa jioni, akiwa maeneo ya Kinondoni, Mkwajuni, jijini Dar es Salaam. Alikuwa kwenye basi la daladala linalotokea Mabibo kwenda Makumbusho.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Akwilina alikuwa ameketi kwenye kiti cha nyuma cha basi alilopanda. Risasi iliyochukua maisha yake, ilitokea nyuma ya alikokuwa.

Kubenea amesema, historia ya Mwigulu inaonyesha kuwa ni mtu wa kukwepa uwajibikaji kwa kutengenezea stori wengine.

Amesema, “Mwigulu amekuwa akikutuhumu Chadema kwenye mikutano ya hadhara na kuihusisha na matukio kadhaa ya uhalifu. Amefanya hivyo, tangu alikiwa naibu katibu mkuu wa CCM, Tanzania Bara.”

Kubenea ametoa orodha ya matukio ambayo Mwigulu ameihusisha Chadema, likiwamo la kumwagiwa tindikali kwa kijana wa Igunga, kushambuliwa kwa risasi kwa mfanya biashara wa magazeti mkoani Morogoro na mauaji ya Daud Mwangosi.

Akiongea kwa kujiamini, Kubenea amesema, “lakini wakati haya yanatokea, aliyekuwa mtendaji mkuu wa chama, ni Dk. Willibroad Slaa, ambaye sasa ameteuliwa na rais Magufuli kuwa balozi. Hii ina maana kuwa Mwigulu anaeneza poropaganda na chuki miongoni mwa wananchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

IFP wakubali kuungana na ANC kuunda serikali

Spread the loveChama cha upinzani nchini Afrika Kusini, Inkatha Freedom Party (IFP)...

BiasharaHabari za Siasa

Prof. Mkumbo: Pato la taifa limefikia trilioni 148

Spread the loveWaziri wa Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema mwaka...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Deni la Serikali lafikia trilioni 91

Spread the loveWaziri wa Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema hadi...

Habari za SiasaTangulizi

Mbunge Dk. Shogo Mlozi afariki dunia

Spread the loveMbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) ambaye pia ni...

error: Content is protected !!