Tuesday , 27 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Akwilina aagwa, wanafunzi watoa neno zito kwa serikali
Habari za SiasaTangulizi

Akwilina aagwa, wanafunzi watoa neno zito kwa serikali

Mwili wa Akwilina Akwilini ukiagwa huku wanafunzi wa NIT wakionesha mabango yenye ujumbe mzito kwa serikali
Spread the love

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo, Prof. Joyce Ndalichako amesutwa na wanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji Tanzania (NIT) baada ya kutaka kuwatetea wauaji wa Akwilina Akwilini. Anaripoti Mwandishi Wetu …. (endelea).

Tukio hilo limetokea leo Alhamisi Viwanja vya NIT, Mabibo jijini Dar es salaam wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Akwilina, aliyeuwawa kwa risasi “iliyorushwa na Polisi” Ijumaa iliyopita wakati wa wafuasia wa Chadema walipokuwa wakielekea kwenye ofisi za Msimamizi wa Uchaguzi Kinondoni kudai fomu za viapo.

MwanaHALISI Online imeshuhudia wanafunzi hao wakinyanyua mabango yanayoashiria kutokukubaliana na utetezi uliokuwa ukitolewa na Prof. Ndalichako kwa niaba ya serikali kuhusiana na kifo cha Akwilini ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika mchuo cha NIT.

Aliyehamsha hisia kali za wanafunzi hao, alikuwa Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam pale alipodai kuwa kifo hakizuiliki na hivyo siku za kuishi za Akwilina duniani zilikuwa zimekwisha.

Maneno hayo ambayo yalionekana kuwakera wanafunzi waliokuwepo viwanjano hapo kwa lengo la kumuaga mwanafunzi mwenzao na kuanza kuibua minong’ono ya chinichini lakini hawajafanya lolote, Makonda alimkaribisha Prof. Ndalichako kuzungumza.

Wanafunzi wa NIT wakionesha mabango yenye ujumbe mzito kwa serikali
Wanafunzi wa NIT wakionesha mabango yenye ujumbe mzito kwa serikali

Prof. Ndalichako alipoanza hotuba yake kulikuwa na utulivu, lakini alitoa kauli ambazo zilikuwa zinaashiria kuwatetea wauaji wa Akwilina, ndipo alipojikuta yupo katikati ya mabango ya wanafunzi hao na kusababisha waombolezaji kuacha kusikiliza anachozungumza na kuangalia kilichoandikwa kwenye mabango hayo.

Wanafunzi walisimama kuonesha mabango yao kwa waandishi wa habari na miongoni mwa ujumbe uliokuwemo kwenye mabango hayo ni ule uliosema, “Tunataka tume huru ya uchunguzi” na mwingine ulisomeka, “Wauaji hawawezi kujichunguza.”

Mbali na mabango hayo ya wanafunzi, lakini Padre aliyekuwa akiongoza misa ya kumuaga marehemu Akwilina, Padre Raymond Mayanga wa Katisa Katoliki Parokia ya Yohana Mbatizaji Mabibo Luhanga, amepigilia msumari baada ya kusema serikali iache ujanja ujanja imtafute aliyempiga risasi iliyosababisha kifo cha Akwilina.

Amesema: “Serikali iache ujanja ujanja. Hiki siyo kipindi cha ujanja ujanja. Hiki ni kipindi cha kufanya toba. Serikali imtafute aliyempiga risasi Akwilina na aombe radhi kwa umma kupitia televisheni.”

Mbali na Akwilina watu wengine kadhaa walijeuruhiwa na risasi na kulazwa katika hospitali mbalimbali ikiwemo Mwananyamala na Muhimbili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Hamahama Ngorongoro kutikisa maandamano ya Chadema Arusha

Spread the loveMAELFU ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na...

Habari za SiasaTangulizi

Waliofariki ajalini Arusha kuagwa siku ya maandamano Chadema

Spread the loveMIILI ya watu 25 waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kuiburuzwa mahakamani ajali iliyoua 25 Arusha

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), imeitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

error: Content is protected !!