Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa DC aagiza mbunge mwingine wa Chadema akamatwe
Habari za Siasa

DC aagiza mbunge mwingine wa Chadema akamatwe

Frank Mwakajoka, Mbunge wa Tunduma
Spread the love

MBUNGE wa Chadema, katika jimbo la Tunduma, mkoani Mbeya, Frank Mwakajoka, amewekwa ndani muda huu kwa amri ya mkuu wa wilaya. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mwakajoka ameswekwa rumande baada ya kuwapiga picha na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii, madiwani watatu wa chama hicho waliojiengua na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Wanadaiwa kupigwa picha na Mwakajoka, ni Ayub Mlimba ambaye alikuwa diwani wa kata ya (Mwaka Kati), Simon Mbukwa (Kaloleni) na Amos Nzunda (Mpemba).

Taarifa zinasema, tukio hilo lilitokea wakati madiwani hao walipoitwa na serikali kuhudhuria kikao cha bajeti cha halmashauri ya Mji Mdogo wa Tunduma, leo Jumatano.

“Hawa watatu wa nyuma ndio waliokuwa madiwani wa Chadema na ambao wamejiuzulu nafasi zao. Lakini leo wameitwa kwenye kikao cha bajeti cha Mji, huku wakiwa wamehama chama na kujiuzulu nafasi zao za udiwani,” ameeleza Mwakajoka katika moja ya ujumbe wake kwa wabunge wenzake.

Muda mfupi baadaye, mbunge huyo anaandika, “…na sasa nawekwa chini ya ulinzi na pia nakaa ndani kwa saa 48 kwa amri ya DC (mkuu wa wilaya).”

Baraza la madiwani la Tunduma linaundwa na Chadema; jambo ambalo linaifanya CCM ambacho ni chama cha upinzani, kutokuridhika na uamuzi huo wa wananchi.

Wote watatu walitangaza kuondoka Chadema, tarehe 6 Februari mwaka huu kwa madai yaleyale ya “kufurahishwa na utendaji kazi wa Rais John Magufuli.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!