Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Kiwango cha deni la Kenya chafikia rekodi ya juu, deni la China latajwa
Kimataifa

Kiwango cha deni la Kenya chafikia rekodi ya juu, deni la China latajwa

Spread the love

pPAMOJA na jitihada za Rais wa Kenya William Ruto za kudhibiti kiwango cha deni la taifa hilo lakini inaripotiwa madeni kufika rekodi za juu. Imeripotiwa na Portal Plus  … (endelea).

Kulingana na takwimu, jumla ya deni la Kenya limepanda kwa rekodi ya dola za Marekani bilioni 10.8 hadi dola za Marekani bilioni 70.75, na kukiuka kiwango cha ukomo wa deni kilichowekwa Juni 2022 na bunge la nchi hiyo huku kiwango cha deni kikivuka cha mwaka uliopita kwa zaidi ya asilimia 18.

Ongezeko la deni la umma lilichangiwa na ulipaji wa mikopo ya nje, kushuka kwa kiwango cha ubadilishaji fedha na kulipwa kwa deni la ndani .

Ripoti hiyo inaeleza kuwa gharama za ulipaji wa mkopo, hasa kwa China, zimepanda wakati sarafu ya nchi hiyo inafanya biashara kwa kiwango cha chini cha karibu shilingi 144 kwa dola.

Gharama ya kulipa deni katika mwaka wa fedha ulioishia Juni ilikuwa dola bilioni 2.7, ambapo malipo ya juu zaidi – shilingi bilioni 107 (USD 743 milioni) – yalikwenda China.

Kwa mujibu wa Website ya The Citizen ulipaji wa deni la Kenya kwa China unaendelea kuongezeka.

Kuongezeka kwa ulipaji wa deni kulitokana na sababu kama vile ukomavu wa baadhi ya mikopo iliyochukuliwa kutoka China. Kwa mfano, Reli ya Standard Gauge (SGR) ilifadhiliwa na mkopo kutoka Benki ya Exim ya China ambao utaiva mwaka wa 2027.

Serikali pia inalipa mikopo iliyochukuliwa kutoka China ili kufadhili miradi mingine ya miundombinu, kama vile upanuzi wa Bandari ya Mombasa na Bandari ya Lamu na Ukanda wa Usafiri wa Lamu-Kusini mwa Sudan-Ethiopia (LAPSSET).

Wabunge wa Kenya kwa hivyo wamepiga kura ya kubadilisha kiwango cha ukomo wa deni hadi sehemu ya pato la taifa (GDP), ingawa marekebisho hayo bado hayajapitishwa na Seneti.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wadukuzi wa Kichana waiba barua pepe 60,000 za Serikali ya Marekani

Spread the loveWADUKUZI wa kichana wamedukua barua pepe 60000 serikali ya Marekani...

Kimataifa

Mahakama yamkuta na hatia Donald Trump

Spread the love  ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, amekutwa na hatia...

Kimataifa

Harusi yageuka msiba 100 wakifariki kwa ajali ya moto

Spread the love  WATU takribani 100, akiwemo bibi na bwana harusi, wamefariki...

Kimataifa

Kampuni ya mali ya China Oceanwide yapata agizo la kufilisiwa huko Bermuda

Spread the love  MAHAKAMA ya Bermuda imetoa amri ya kufilisiwa kwa Kamapuni...

error: Content is protected !!