Tuesday , 26 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia apangua tena Manaibu Mawaziri, Mnyeti ahamishwa kabla ya kuapishwa
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia apangua tena Manaibu Mawaziri, Mnyeti ahamishwa kabla ya kuapishwa

David Silinde, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amefanya
uhamisho na uteuzi wa viongozi mbalimbali ikiwamo Naibu Waziri David Silinde ambaye amehamishwa kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenda kuwa Naibu Waziri wa Kilimo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Sakaam …(endelea).

Aidha, Alexander Mnyeti ambaye mapema leo ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo, jioni hii amehamishiwa katika nafasi ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi.

Katika taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu leo Jumatano jioni, pia Rais Samia amemteua Balozi Mhandisi Aisha Amour kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi.

Katika taarifa hiyo pia ameteua Wajumbe wanne wa Tume ya Mipango.

Wajumbe hao ni Balozi Ombeni Yohana Sefue – Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu na Omar Issa – Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO na Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandela.

Wengine ni Balozi Ami Ramadhan Mpungwe – Balozi Mstaafu na Mịasiriamali na Maryam Salim- Mencja Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Cambodia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Habari za Siasa

Kamugisha aanika utekelezaji mpango kazi 2022/23

Spread the loveMWENYEKITI wa Ngome ya Vijana ya Chama Cha ACT-Wazalendo Mkoa...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo wakabidhiwa kivumbi kulinda kura uchaguzi 2024,2025

Spread the loveNGOME ya Vijana ya Chama cha  ACT-Wazalendo, imetakiwa kuwanoa wafuasi...

error: Content is protected !!