Tuesday , 26 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yataka Serikali kutumia mbinu za kisayansi kudhibiti uvamizi wanyama pori
Habari za Siasa

Chadema yataka Serikali kutumia mbinu za kisayansi kudhibiti uvamizi wanyama pori

Mbowe akihutubia wananchi
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeitaka Serikali kutumia mbinu za kisayansi kudhibiti uvamizi wa wanyamapori katika maeneo wanaoyoishi wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Simiyu…(endelea).

Wito huo umetolewa leo tarehe 30 Agosti 2023 na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, akizungumza katika mkutano wa hadhara wa chama hicho, kwenye Jimbo la Kisesa, mkoani Simiyu.

“Wale wanyama wanafuta mlo, kwa bahati mbaya wanaishi jirani na makazi ya watu. Tatizo sio la wanyamapori wala wananchi, tatizo ni viongozi wa Serikali walioshindwa kutengeneza mikakari na mbinu za kuwadhibiti wanyama ili waishi katika mahusiano mema na jamii ya wananchi waliopakana na hifadhi,” amesema Mbowe.

Mbowe ameitaka Serikali kuiga mfano kutoka nchi jirani zenye mbuga za wanyamapori, wanaotumia mbinu za kisayansi ikiwemo kujenga kuta za umeme.

“Nimesema sera ya CCM kuhusu kudhibiti kuhama na kuhifadhi wanyama hakujafanyika kisayansi, kunafanyika kama vile wakati Mungu anaumba dunia. Maisha ya leo sayansi inakwenda mbele sana na chukua mfano wa Kenya ukienda hutakuta hata siku moja anatoka fisi anawaumiza wananchi sababu wameweka mfumo wa kuwalinda raia kwa kuweka fensi za umeme,” amesema Mbowe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Habari za Siasa

Kamugisha aanika utekelezaji mpango kazi 2022/23

Spread the loveMWENYEKITI wa Ngome ya Vijana ya Chama Cha ACT-Wazalendo Mkoa...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo wakabidhiwa kivumbi kulinda kura uchaguzi 2024,2025

Spread the loveNGOME ya Vijana ya Chama cha  ACT-Wazalendo, imetakiwa kuwanoa wafuasi...

error: Content is protected !!