NAIBU Waziri wa Fedha, Hamadi Chande amesema serikali inatarajia kuja na mpango wa kuwezesha wafanyabiashara wa Tanzania na China kutumia sarafu ya Tanzania kununua bidhaa nchini China. Anaripoti Maryam Mudhihiri na Mlelwa Kiwale…(endelea).
Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande ameyasema hayo leo tarehe 30 Agosti 2023, bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi (CCM) aliyetaka kufahamu iwapo serikali ipo tayari kuandaa mazingira ya kuwezesha biashara kati ya China na Tanzania kufanyika kwa shillingi.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri huyo, amesema kuwa serikali itaifanyia kazi jambo hilo ili kuona ni nini kinafanyika kuwezesha bishara ya China kukubali matumizi ya sarafu ya Tanzania.
“Katika biashara za kitaifa wafanyabiashara wanaouhuru wa kutumia sarafu yoyote inayorahisisha biashara zao inayokubalika na nchi nyingine kwa lengo la kupunguza gharama za miamala na muda,” amesema.
Leave a comment