Serikali ya Zambia imetangaza kuahirisha kuanza kwa muhula mpya ya masomo kwa wiki tatu zaidi kutokana mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambao umeshaua watu 150 tangu Oktoba, 2023. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea).
Waziri wa Elimu nchini humo, Douglas Syakalima amesema shule nchini humo zilipaswa kufunguliwa tarehe 8 Januari 2024 lakini sasa zitafunguliwa tarehe 29 Januari 2024.
Zaidi ya watu 4,000 wameugua kipindupindu na vifo 150 vimeripotiwa, takwimu za hivi karibuni za Serikali zinaonyesha kiwango cha vifo ni asilimia 3.7.
“Serikali ina wasiwasi kuhusu athari za mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika sekta ya elimu, hivyo hatua hiyo imechukuliwa ili kulinda afya za wanafunzi,” amesema Syakalima.
Leave a comment