Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kinara wa mtandao wa dawa za kulevya akamatwa Boko
Habari za Siasa

Kinara wa mtandao wa dawa za kulevya akamatwa Boko

Spread the love

Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya Tanzania (DCEA) imemkamata kinara wa mtandao wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya aina ya Cocaine.

Pia imekamata kilogramu 692,336 za dawa hizo na watuhumiwa wengine wa nne. Anaripoti Mwandishi Wetu … endelea.

Akizungumza na waandishi wa habari leo 25 Januari 2024 jijini Dar es salaam na Kamishna Jenerali, Aretas Lyimo amesema kinara huyo aliyekua anatafutwa muda mrefu, amekamatwa maeneo ya Boko wilaya ya Kinondoni.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya Tanzania (DCEA), Aretas Lyimo

Amesema kinara huyo amekamatwa na wenzie watatu huku mmoja akikamatwa wilaya ya Mbeya mkoa wa Mbeya kijiji cha Shamwego.

“Huyu mfanyabiashara ni mkubwa kwa wiki anauwezo wa kusafirisha watu 10 ‘punda’ kwa ajili ya kusambaza dawa hizo maeneo mbalimbali duniani… kibaya zaidi anatumia watoto wa maskini kuwabebesha dawa hizo na hatimaye wengine wanafia njiani,” amesema Kamishna Jenerali Lyimo.

Aidha, Kamishna Lyimo amefafanua kuwa dawa hizo aina ya Cocaine huzalishwa kwa wingi katika bara la Amerika kusini na kusafirishwa kwa njia ya anga na wabebaji ni ‘Punda’.

Amesema watu hao humeza dawa hizo kwa mfumo wa pipi ambapo mtu mmoja anabeba kilogramu 300 mpaka 1200 na wengine hubeba hadi gramu 2000 kwa wakati mmoja.

“Huyu mfanyabiashara tuliyemkamata ana mtandao mkubwa wa wabebaji (punda) kutoka nchi mbalimbali hivyo makosa yake yanaangukia katika uhalifu wa kupangwa unaovuka mipaka,” amesema Kamishna Jenerali Lyimo.

Sambamba na hayo Kamishna Lyimo ametangaza operesheni kali mwaka huu 2024 ya kupambana na dawa za kulevya ambapo itafanyika nchi kavu na baharini.

Amesema kwa nchi kavu oparesheni hiyo itahusisha mashamba ya dawa hizo, mipaka na kwenye maeneo yote ya kusambazia ikiwemo vijiwe vya usambaji na watumiaji.

Akizungumzia oparesheni baharini amesema itahusisha fukwe na katikati ya bahari lakini pia kwenye maeneo yote yanayouza shisha.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!