Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kinana awaachia maswali Watanzania kuhusu Mwalimu Nyerere
Habari za Siasa

Kinana awaachia maswali Watanzania kuhusu Mwalimu Nyerere

Spread the love

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amewataka Watanzania wajiulize kwa nini Tanzania inaendelea kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere licha ya kufariki dunia, tofauti na nchi nyingine za Kiafrika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Swali hilo lilitolewa na Kinana, leo Jumamosi, tarehe 23 Aprili 2022, akizungumza katika sherehe za kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa Mwalimu Nyerere, zilizofanyika nyumbani kwake Msasani, jijini Dar es Salaam.

“Tuna nchi 54 za kiafrika, ni vizuri mfanye utafiti kujaribu kugundua katika hizo nchi ambazo zilikuwa na viongozi tangu uhuru mpaka leo, ngapi zinaendelea kuthamini kiongozi wao wa kwanza? Kwa kadri ninavyofahamu ni mbili, Tanzania na Afrika Kusini, vizuri kujiuliza ni kwa nini?” amesema Kinana.

Aidha, Kinana amesema Watanzania wanamkumbuka Mwalimu Nyerere kutokana na msimamo wake wa kujali utu na ubinadamu.

“Swali la pili ambalo ningependa tujiulize, ameacha uongozi wa nchi miaka 40 iliyopita, amefariki karibu miaka 30 iliyopita. Kwa nini bado tunamkumbuka, yuko kwenye mioyo na midomo yetu? Nadhani sababu ambazo tunaweza kuzigundua zinahusiana na maneno ambayo mara kwa mara yanarudiwa, utu na ubinadamu,” amesema Kinana.

Kada huyo mkongwe wa CCM, amesema chama chake kitaendelea kufuata misingi iliyoasisiwa na Mwalimu Nyerere enzi za uhai wake.

“Wote mnafahamu Mwalimu Nyerere alikuwa muasisi wa chama chetu cha TANU baadae CCM, tunapoazimisha miaka 100 ya kuzaliwa kwake, tunatambua mchango wake mkubwa kwa chama chetu. Tutaendelea kufuata, kuzingatia misingi imara aliyotuachia,” amesema Kinana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!