MAKAMU Mwenyekiti wa chama tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM)-Bara, Abdulrahman Kinana ametangaza ziara ya kichama ya mikoa minne atakayoifanya hivi karibuni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kinana ametangaza ziara hiyo leo Jumapili, tarehe 10 Aprili 2022, katika ukumbi wa Diamond Jubelee wakati CCM Mkoa wa Dar es Salaam walipomwandalia mapokezi rasmi, baada ya kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo.
Alichaguliwa na mkutanomkuu maalum tarehe 1 Aprili 2022 jijini Dodoma, akichukua nafasi ya Philip Mangula aliyetangaza kung’atuka, mara baada ya kukitumikia chama hicho kwa nafasi mbalimbali kwa kipindi kirefu.
Kinana aliyewahi kuwa katibu mkuu wa chama hicho amesema, mara baada ya kuingia ofisini na kuzoea mazingira na majukumu yake, “nitafanya ziara katika mikoa ya Pwani, Tanga, Kilimanjaro na Arusha.”
“Baada ya kumaliza mikoa hii minne, nitaanza ziara ya mikoa mingine saba kwa mpigo. Lazima chama chetu kiwe imara na tusipokuwa na chama imara kama alivyosema Mwalimu Nyerere Taifa letu litayumba.”
Hata hivyo, Kinana hakubainisha mikoa hiyo mingine saba kwa majinga ingawa amesema, wakati ukifika atajulisha.
Leave a comment