Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kilowati 100 mradi wa Bwawa la Nyerere zaingizwa gridi ya Taifa
Habari za Siasa

Kilowati 100 mradi wa Bwawa la Nyerere zaingizwa gridi ya Taifa

Spread the love

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko ameeleza kuridhishwa na kazi inayofanywa na wakandarasi pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika ujenzi wa mradi wa ya mradi wa umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) baada ya kuelezwa kuwa majaribio ya mtambo namba 9 katika mradi wa JNHPP yameleta mafanikio na kilowati 100 zimeanza kuingizwa gridi ya Taifa. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumapili na Makamu wa Rais wa kampuni ya Elsewedy, Mhandisi Wael Hamdy katika mazungumzo ya Dk. Biteko na Waziri wa Nyumba, Nishati na Maendeleo ya Makazi wa Misri, Assem Elgazzar.

Kikao hicho kilijikita kuzungumzia maendeleo ya mradi wa umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) ambao kwa sasa umefikia asilimia 95.83.

Waziri wa Misri aliongozana na watendaji wakuu wa kampuni ya JV Elsewedy na Arab Contractors (wanaotekeleza mradi wa JNHPP).

Kwa upande wa Tanzania viongozi waliohudhuria ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga.

“Kikao hiki kimejikita kuzungumzia masuala mbalimbali kuhusu mradi wa JNHPP, Waziri Elgazzar ametumwa na Rais wa Misri kwa ajili ya kuona maendeleo ya mradi huu.

“Jambo lililotufurahisha hapa ni majaribio ya mtambo namba Tisa yanaendelea na kwa hatua ya mwanzo ambayo wamejaribu kuzungusha mtambo kwa njia ya maji wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa na wameingiza kilowati 100 kwenye gridi ya Taifa,” amesema Dk. Biteko

Ameeleza kuwa, mafanikio ya majaribio hayo yanaleta matumaini kwani ratiba ya kazi inaenda mapema zaidi ya iliyopangwa mwanzo na hii ni kutokana na kazi nzuri ya Wakandarasi pamoja na TANESCO na kwamba lengo ni kuzalisha megawati 235 kutoka mtambo namba 9 ifikapo Februari mwaka huu na kuendelea na mitambo mingine ikiwemo mtambo Namba 8 na Namba 7.

 

Ameongeza kuwa, mradi huo ni wa kipaumbele cha Rais Samia Suluhu Hassan ili watanzania wapate umeme wa uhakika kwa kuwa mradi huo ukimalizika utaingiza megawati 2115 katika gridi ya Taifa.

Amesema kuwa, katika kikao hicho wamezungumza pia kuhusu masuala fedha zilizotengwa kwa ajili ya huduma za kijamii zinazotokana na uwepo wa mradi huo ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya mkataba.

Katika hatua nyingine, Dk. Biteko ameomba Watanzania wawe na subira wakati Serikali ikitekeleza miradi mbalimbali itakayoongeza kiasi cha umeme nchini ikiwemo mradi huo wa JNHPP.

Vilevile amesema kuwa, mradi wa JNHPP ni wa kielelezo kwa Afrika kwani inaonesha kuwa nchi za Kiafrika zinaweza zenyewe kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati.

Kwa upande wake, Waziri wa Nyumba, Nishati na Maendeleo ya Makazi wa Misri, Assim Elgazzar amesema kuwa nia ya Serikali hiyo kutoka mwanzo ni kuona kuwa mradi huo unakamilika kwa ufanisi na kwa wakati na amewapongeza wakandarasi pamoja na TANESCO kwa hatua nzuri ya utekelezaji wa mradi huo.

Amesema kuwa, Serikali ya nchi hiyo itaendelea kuwapa ushirikiano Wakandarasi hao katika hatua zote za utekelezaji wa mradi na kueleza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutatoa fursa kwa kampuni za nchi hizo kuendelea kuaminika kwenye utekelezaji wa miradi mingie ikiwemo ya umeme.

1 Comment

  • Duh! Kwa nini tunaendelea na ubabaishaji. Kama hili bwawa lingejengwa na Wajapani au Wakorea ya kusini lingeshakuwa linazalisha umeme 100% kwa sasa! Hatuhitaji visingizio vya umaskini, hali ya uchumi, n.k.
    Sijawahi kuona wawili Hao wamesitisha ujenzi namna hii!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!