Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kidata awataka watumishi TRA kuzingatia maadili, uaminifu
Habari Mchanganyiko

Kidata awataka watumishi TRA kuzingatia maadili, uaminifu

Spread the love

 

KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata amewaagiza watumishi wa mamlaka hiyo kuwa mfano bora kwa wengine kwa kuzingatia maadili na kuonyesha kuwa kwa pamoja wanaweza kulipa kodi na kukusanya mapato ya Serikali kwa ufanisi na uaminifu ili kulijenga Taifa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Pia amewataka watumishi hao kujitahidi kuwa wakweli na waadilifu katika kazi zao, na wajitahidi kuwajibika ili kuleta matokeo chanya kwa jamii.

Kamisha Kidata ametoa kauli hiyo katika hafla ya futari pamoja na watumishi na wadau wa mamlaka hiyo iliyofanyika jana Ijumaa jijini Dar es Salaam.

Amesisitiza kuwa TRA itaendelea kushirikiana na kufanya kazi kwa bidii na kwa dhati kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu.

“Sisi, kama watumishi wa umma, pamoja na wadau wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, tuna jukumu la kuhakikisha kuwa tunalitumikia taifa letu kwa uaminifu na kwa kuzingatia maadili yetu ya kitanzania, sheria, kanuni, na taratibu za kazi zetu.

“Wakati huu wa funga ya Ramadhan, ni wakati mzuri wa kufanya tafakari juu ya matendo yetu ya kila siku kwa kuzingatia wajibu wetu wa kulipa kodi kama wananchi wenye uzalendo na nchi yetu, na jukumu letu la ukusanyaji wa Mapato ya Serikali kwa maendeleo ya taifa letu,” amesema.

Amesema kwa kuzingatia utukufu wa mwezi huu wa Ramadhani, ni vyema wakazidisha ibada, kuzingatia na kuimarisha umoja na mshikamano walionao, kuwasaidia kwa moyo wale wote wenye uhitaji, pamoja na kuzidisha huruma na upendo kwa kila mmoja.

Awali akitoa mawaidha, Sheikh Juma Dadi alisema katika kipindi hiki cha mfungo wanaelekezwa umuhimu wa kuzingatia maadili.

Alisema katika kipindi hiki kumekuwepo na mmomonyoko mkubwa wa maadili katika pande mbalimbali kuanzia taasisi za serikali na watumishi.

“Kumekuwepo na. utovu wa maadili hasa baadhi ya watu katika sekta walipo. Kwa utovu wa maadili watu wamekuwa wakikosa haki katika kupata huduma za msingi badala yake watoa huduma wanataka rushwa. Wanafichaficha wanasema takrima.

“TRA pia wanalalamikiwa sana kutokana na utoaji huduma mara nyingi wananchi wanaambiwa hakuna mtandao wakati ni kwa makusudi lengo ni kuchelewesha watu ili kutengeneza mazingira ya rushwa. Wapo wachache wanaoharibu sifa ya taasisi mnayotumikia, hivyo ni lazima kuliangalia hili,’ alisema Sheikh Dadi ambaye alimuwakilisha Sheikh wa Wilaya ya Ilala Sheikh Adam Mwinyipingu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!