Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kesi ya wanandoa kujeruhi jirani yapigwa kalenda tena
Habari Mchanganyiko

Kesi ya wanandoa kujeruhi jirani yapigwa kalenda tena

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imeahirisha kesi ya kujeruhi na kutoa lugha ya matusi inayomkabili wanandoa Bharat Nathwan (57), Sangita Bharat (54) hadi Mei 2 ,2024 kwa sababu ya kutokuwepo kwa wakili wa washitakiwa hao mahakamani kwa taarifa kwamba amefiwa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Wanandoa hao ambao ni raia wa Tanzania asili ya kihindi wanaoishi Mtaa wa Mrima – Kisutu, jingo la Lohana Dar es Salaam wanaotuhumiwa kwa mashitaka manne waliyoyatenda Julai 21,2023 kinyume cha sheria.

Taafifa hiyo ilitolewa na Wakili  wa Serikali Mwandamizi, Grace Mwanga akisiadiana na Frank Michael mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Aaron Lyamuya wa mahakama hiyo, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa kwa shahidi wa tatu wa upande wa mashitaka.

Mkazi wa Dar es Salaam Bharat Nathwan mwenye shati jeusi akisubiri kuingia kwenye kesi yake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana jijini Dar es Salaam kusikiliza kesi inayomkabili ambapo anatuhumiwa kumjeruhi jirani yake Lalit Kanabar kwa kumpiga vichwa.

“Mheshimiwa kesi ilikuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa, lakini hatukumleta shahidi kwa sababu tulipokea barua kutoka kwa wakili wa washitakiwa kwamba hatofika mahakamani kwa sababu amefiwa kwa hiyo tunaomba ahirisho la kesi hii,”alidai Mwanga

Baada ya ombi hilo kutolewa, Hakimu Lyamuya alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Mei 2, 2024 kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.

“Washitakiwa mnasikia kesi yenu itaendelea kusikilizwa Mei 2, mwaka huu kama mlivyosikia taarifa iliyotolewa na wakili wa serikali,”alisema Hakimu Lyamuya

Awali, Fundi Seremala, Dominic Mpakani (43) aliileza mahakama jinsi mshitakiwa Bharat Nathwan allivyomshambulia jirani wake, Lalit Ratilal kwa kumpiga kichwa kifuani kisha akadondoka chini na nakupoteza fahamu kwa muda.

Sangita Natwani ambaye anashtakiwa na mume wake Natwani kwa kumjeruhi jirani yao

Aidha, alidai kuwa kulikuwa na ugomvi kati ya mke wa Bharat (Sangita Bharat) na mke wa Lalit, (Kiran) ambao walikuwa wakirushiana maneno kwa ukali kwa lugha ya kihindi huku, baada ya muda kidogo waume zao walifika kwa pamoja na kuingilia ugomvi huo.

Alidai kuwa Julai 21,2023 alikuwa nyumbani kwa Lalit Ratilal maeneo ya mtaa wa Mrima katika jingo la Lohana, alimuita kwa ajili ya kuifanyia kazi zinazohusiana na mbao na kazi zingine ndogo ndogo.

Alidai kuwa alifika katika jengo hilo saa tatu asubuhi ambapo bosi wake huyo anakaa floor ya tatu, wakati anaendelea na kazi alidai kuwa Sangita alikuwa amesimama kwenye dirisha lake na Kiran alikuwa amesimama kwenye mlango wake, kila mmoja alianza kuzungumza kwa ukali na kwa jaziba wakitumia lugha ya kihindi.

“Lakini nilimsikia mke wa Bharat, Sangita akimwambia mke wa Lalit kwamba uchafu wake apeleke huko ambapo vitu vyote vilikuwa vimewekwa katika eneo la Lalit na hakuna kitu chochote kilichokuwa katika eneo la Sangita. Baada ya dakika kadhaa sijui walipiga simu au vipi waume zao walikuja kwa wakati mmoja na malumbano yakaendelea kwa wote wanne,” alidai Fundi Mpakani

Shahidi huyo alidai kuwa, wakati malumbano hayo yanaendelea wote walikuwa wamesimama kwenye mlango wa Lalit, baada ya muda Bharat akampiga kichwa Lalit na Lalit akadondoka chini na kupoteza fahamu.

Shahidi mwingine ambae ni Dk Lucia Augustino (52) wa Hospitali ya Mnanzi Mmoja alidai kuwa Julai 21,2023 alikuwa Idara ya Dharura chumba namba  20 muda wa mchana alipokea wateja wawili wenye asili ya kiashia walikuwa wamechafuka kuanzia kichwani hadi miguuni , mama alichafuka sana kuliko baba.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, washitakiwa hao ambao ni raia wa Tanzania jinsia ya kihindi wanaoishi Mtaa wa Mrima – Kisutu, jengo la Lohana Dar es Salaam wanaotuhumiwa kwa mashitaka manne waliyoyatenda Julai 21,2023.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!