Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kesi ya Tito VS NEC: Mahakama yaipa siku nne Jamhuri
Habari Mchanganyiko

Kesi ya Tito VS NEC: Mahakama yaipa siku nne Jamhuri

Wakili Tito Magoti, Mtumishi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)
Spread the love

 

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imetoa siku nne kwa upande wa Jamhuri kuwasilisha hati kinzani, katika kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na mtetezi wa haki za binadamu, Tito Magoti na mwenzake, kupinga mahabusu kunyimwa haki ya kushiriki uchaguzi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Amri hiyo imetolewa leo Jumatatu, tarehe 7 Machi 2022 mahakamani hapo, mbele ya Jaji John Mgetta, wakati kesi ilipokuwa inatajwa.

Upande wa Jamhuri umeamriwa kuwasilisha hati kinzani kwa maandishi mahakamani hapo tarehe 11 Machi 2022, kisha upande wa wadai utaijibu tarehe 18 Machi mwaka huu, wakati kesi hiyo itakapokwenda kutajwa.

Jaji Mgetta alitoa amri hiyo baada ya upande wa Jamhuri, kuomba muda wa kuwasilisha hati hiyo.

Jamhuri iliwakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nalindwa Sekimanga, Emmanuel Kawishe, kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Inspekta wa Polisi kutoka Jeshi la Magereza nchini, Zabron Simion.

Huku upande wa wadai ukiwakilishwa na Wakili John Seka na Paul Kisabo.

Tito na mwenzake, John Tulla, wamefungua kesi hiyo namba 3/2022, dhidi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) na Jeshi la Magereza.

Mahakama Kuu ya Tanzania

Katika kesi hiyo iliyofunguliwa tarehe 28 Februari 2022, Tito anaiomba mahakama itoe amri kwa NEC na wenzake, ilimpe fidia kwa kushindwa kumuwekea mazingira yeye na mahabusu wenzake, kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Tito na mwenzake wanadai kuwa, NEC imepewa mamlaka chini ya Ibara ya 5 (1) ya Katiba, kuhakikisha kila raia mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea, anayekidhi vigezo kwa kushiriki uchaguzi, anapewa haki ya kupiga kura katika uchaguzi.

Mwanaharakati huyo na mwenzake wanadai kuwa, NEC ilikiuka misingi ya katiba katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, kwa kutowaandikisha mahabusu walioko magereza wakisubiri usikilizwaji wa kesi zao, kwenye daftari la wapiga kura.

Tito na mwenzake wanadai kuwa, kitendo cha wao kutopiga kura wakiwa mahabusu, kimewaathiri moja kwa moja.

Kwenye kesi hiyo, Tito na mwenzake, wanaiomba mahakama itamke kuwa, masharti ya kifungu cha 11 (1) (C), cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, hayaendani na matakwa ya kifungu cha 5 (2) (C) cha katiba.

Pia, wanaiomba mahakama itamke kwamba, wafungwa wanaotumikia kifungo cha zaidi ya miezi sita, kuwa wanastahiki na wana haki ya kuandikishwa kama wapiga kura katika daftari la kudumu la wapiga kura, kalba ya Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!