October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya Mbowe: Jamhuri yaondoa mashahidi 4, mshtakiwa aanza kujitetea

Spread the love

 

UPANDE wa Jamhuri kwenye kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ya uhujumu uchumi, inayomkabili kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, Freeman Mbowe na wenzake umefunga ushahidi wake. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ni baada ya wakili mwandamizi wa serikali, Robert Kidando kuieleza Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, iliyopo Mawasiliano mkoani Dar es Salaam, kuwa wanaondoa mashahidi wanne kati ya saba iliyopanga kuwatumia.

Tayari mashahidi watatu walikwisha kutoa ushahidi mahakamani hapo kwenye kesi ndogo akiwemo Kamanda wa Polisi wa Kinondono (RPC), Ramadhan Kingai na leo Ijumaa, tarehe 24 Septemba 2021, ilikuwa aendelee shahidi wa nne.

Wengine walitoa ushahidi; ni Inspekta Mahita Omari Mahita na Askari Polisi, Ricado Msemwa.

Hata hivyo, Jaji anayesikiliza kesihiyo, Mustapha Siyani alipomwita wakili wa serikali baada ya pande zote mbili kutambulisha mawakili wao alisema, wanaomba kuwaondoa mashahidi wanne kati ya saba.

Baadaye Jaji Siyani aliuliza upande wa utetezi kama wana lolote la kuzungumza, ambapo Wakili John Mallya alisema wao watatumia mashahidi watatu akiwemo mshitakiwa namba mbili Adam Kasekwana wapo tayari kuanza kwautetezi.

Jaji Siyani aliwauliza kama wanahitaji muda zaidi wa kujiandaa na Wakili Mallya aliieleza mahakama habapana, wako tayari kuanza na kwa sasa Kasekwa yupo kizimbani anatoa ushahidi wake.

Mbali na Mbowe na Kasekwa, washtakiwa wengine ni, Halfan Bwire Hassan na Mohammed Abdillah Ling’wenya.

Katika moja ya swali aliloulizwa Kasekwa wakati akitoa ushahidi na Mallya alikuwa nani.

Kasekwa amesema alikuwa askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikosi namba 72 Sangasanga mkoani Morogoro.

Alipoulizwa ni kikosi cha namna gani amejibu akisema ni kikosi cha makomandoo lakini sasa kinaitwa ‘special force.’

Akijibu swali aliloulizwa kwamba amehudumu nafasi hiyo kwa kipindi gani amesema miaka sita kati ya mwaka 2012 hadi 2018.

Anaendelea kutoa ushahidi…

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

error: Content is protected !!