Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ya Mbowe, wenzake: Jamhuri kuleta shahidi wa nne 
Habari za SiasaTangulizi

Kesi ya Mbowe, wenzake: Jamhuri kuleta shahidi wa nne 

Freeman Mbowe akiwasili mahakamani Kisutu
Spread the love

 

KESI ndogo katika kesi ya uhujumi uchumi, yenye mashtaka ya kula njama za kufanya vitendo vya ugaidi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, inatarajiwa kuendelea kusikilizwa leo Ijumaa, tarehe 24 Septemba 2021. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi ya msingi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya ugaidi ni, Halfan Bwire Hassan, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Ling’wenya.

Kesi hiyo inaendelea kusikilizwa katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam, mbele ya Jaji Mustapha Siyani.

Upande wa Jamhuri unatarajiwa kuleta mahakamani hapo shahidi wake wa nne, kati ya saba katika kesi hiyo ndogo, iliyotokana na mapinganizi ya Mawakili wa utetezi, wakiongozwa na Peter Kibatala.

Wakipinga maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa pili katika kesi ya msingi, Adam Kasekwa, yasitumike mahakamani hapo kama kielelezo katika kesi ya msingi, wakidai yalichukuliwa nje ya muda kisheria.

Pia, mtuhumiwa alichukuliwa maelezo pasina ridhaa yake.

Kabla kesi hiyo ndogo haijaahirishwa Jumatatu iliyopita, mashahidi watatu wa Jamhuri, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kinondoni, ACP Ramadhan Kingai, Inspekta Mahita Omari Mahita na Askari Polisi, Ricado Msemwa, walitoa ushahidi wao mahakamani hapo.

Katika ushahidi wao, mashahidi hao mbele ya mahakama hiyo walieleza namna washtakiwa wawili, Kasekwa na Ling’wenya walivyokamatwa maeneo ya Rao, Moshi mkoani Kilimanjaro hadi walivyofikishwa katika Kituo cha Polisi cha Kati Dar es Salaam na kuhojiwa.

Walidai watuhumiwa hao walipatiwa haki zao za msingi, ikiwemo kujulishwa tuhuma zao na kuchukuliwa maelezo ya onyo kwa hiari yao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

error: Content is protected !!