RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amesema nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), zina uhuru wa kisiasa, lakini zinahitaji uhuru wa kiuchumi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).
Rais Kenyetta amesema hayo akizungumza katika mkutano wa wakuu wa nchi za EAC, leo Alhamisi, tarehe 21 Julai 2022, jijini Arusha.
“Tuna uhuru wa kisiasa, lakini tunahitaji uhuru wa kiuchumi. Tuwe tunajitegemea na tunahitaji kuboresha miundombinu ili soko letu lwie kubwa zaidi,” amesema Rais Kenyatta.
Rais huyo wa Kenya, amezitaka nchi za jumuiya hiyo kutumia vyema rasilimali zake katika kujikomboa kiuchumi.
Duh!
Ukitaka uhuru wa uchumi, kwanza uza mali zisizo zako.
Viongozi wengi wa Afrika ni matajiri kwa sababu wanaiba kwa kalamu.(white collar theft).
Pia, muache kuiibia Tanzania madini, mazao na utalii wake.
Duh!
Mbona mumempiga vita Rostam Aziz?
Biashara makampuni hamsini kwa hamsini. Tunataka hivyo, kwa sababu 2/3 ya nchi yako ni jangwa-usu. Hivyo, unategemea kuinyonya Tanzania.
Watanzania tuache kuwa mabwege wa wakenya.