August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wakuu wa EAC wataka miundombinu bora kuwezesha soko huru

Spread the love

 

WAKUU wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wamesema ili mataifa hayo yaendelee inatakiwa kuwe na miundombinu bora ya usafirishaji pamoja na soko huru. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Kauli hizo zimetolewa na wakuu ha oleo Alhamisi, tarehe 21 Julai 2022, katika mkutamno wa kawaida wa 22 wa wakuu wa nchi za EAC, uliofanyika jijini Arusha.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema ili nchi hizo ziendelee zinatakiwa kuimarisha miundombinu yake pamoja na urari wa biashara.

“Tuwe na namna ya kuweka miundombinu ya barabara zetu ili tuweze kupeleka mazao yetu kutoka kwa wakulima mpaka kwenye masomo yetu au kwenye maghala. Lazima tuangalie namna ya kufanya. Soko ni muhimu sana tunatakiwa tuangalie urari wetu umekaaje katika soko,” amesema Rais Samia.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amesema ili nchi za EAC ziondokane na utegemezi, zinatakiwa kuboresha na kupanua wigo wa miundombinu hususan ya usafirishaji.

“Tunatakiwa kuendelea kujikita katika ujenzi wa miundombinu hata wakituambia tunatumia fedha nyingi kwenye miundombinu tuseme sawa. Wanatamani tuwe wategemezi lakini tunahitaji tujitegemee tusiwe wategemezi,” amesema Rais Kenyetta.

Akizungumza katika mkutano huo, Rais wa Uganda, Yoweri Museven, amesema ili watu wa jumuiya hiyo wapate mafanikio inatakiwa kuwe na soko huru.

“Lazima tuangalie hapa, soko liwe huru kama soko liko huru mfano Tanzania wanazalisha maharage mengi na mpunga, wanatakiwa wajikite katika eneo hilo. Mwingine anaweza akazalisha vizuri upande mwingine, ndiyo kitu tunatakiwa tulinde watu wetu,” amesema Rais Museveni.

error: Content is protected !!