Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kenya yairuhusu Air Tanzania kusafirisha mizigo yake
Habari Mchanganyiko

Kenya yairuhusu Air Tanzania kusafirisha mizigo yake

Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL)
Spread the love

 

Mamlaka ya anga nchini Kenya imeiruhusu kampuni ya ndege nchini Tanzania Air Tanzania kusafirisha mizigo yake kutoka Kenya hadi mataifa mengine kuanzia leo tarehe 16 Januari 2024. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Hatua hii inajiri baada ya Mamlaka ya anga nchini Tanzania kuizuia kampuni ya ndege ya Kenya Airways KQ kuhudumu jijini Dar es Salaam baada ya Kenya kuizuia kampuni ya ndege ya Air Tanzania kusafirisha mizigo kutoka nchini humo hadi mataifa mengine.

Kuafutia uamuzi huo wa Kenya, mamlaka ya anga nchini Tanzania imetangaza kuondoa uamuzi wake wa kuizuia kampuni ya ndege nchini Kenya KQ, kuingia mjini Dar es Salaam mara moja.

Awali Waziri Mkuu wa Kenya, Musalia Mudavadi ambaye pia ndiye Waziri wa mashauri ya kigeni aliandika kwenye akaunti yake ya mtandao wa ‘X’ kuwa alikuwa amefanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, January Makamba na kwamba nchi zote mbili zilikuwa tayari kutatua suala hilo ndani ya siku tatu.

Kwa upande wake, Waziri Makamba aliandika kwenye akaunti yake ya ‘X’ kuwa mamlaka katika nchi zote mbili zilikuwa zimejitolea kutatua suala hilo kwa mujibu wa makubaliano yaliyopo.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Tanzania ilikuwa imetangaza kusitisha safari za ndege za abiria za Shirika la Ndege la Kenya (KQ) kuanzia tarehe 22 Januari mwaka huu.

Hatua hiyo inakuja baada ya Mamlaka ya Ndege nchini Kenya kukataa ombi la Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kuruhusu ndege ya mizigo ya Air Tanzania kusafirisha mizigo kutoka Nairobi kwenda mataifa mengine.

Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Hamza Johari aliiambia BBC kuwa, uamuzi wa Tanzania ulitokana na vikwazo vinavyowekwa na mamlaka za Kenya kuzuia shughuli za ndege ya abiria ya Air Tanzania.

Johari alisema, “Sababu za kuzuia ndege zao ni za msingi, KQ inakuja kwetu (Tanzania) bila vikwazo, lakini sisi ndege yetu ya Air Tanzania inawekewa vikwazo kinyume na makubaliano yetu ya kibiashara ya huduma za ndege tuliyosaini Novemba mwaka 2016.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa wamekuwa wakitafuta mamlaka ya Kenya kwa ajili ya usuluhishi bila mafanikio.

“Tumewaandikia barua hawajibu, pia tumekutana nao bila mafanikio. Lakini kama wakitaka tubadili uamuzi wetu, basi waje mezani tukubaliane juu ya vikwazo vilivyopo kwani mpaka sasa tumepata hasara. Mfano kwa safari moja ya ndege ya mizigo tunapata hasara ya dola za kimarekani 330,000,” alisema Johari.

Mwaka 2020, mamlaka za Tanzania zilisimamisha safari za KQ kati ya Nairobi na viwanja vya Tanzania kama Dar es Salaam, Kilimanjaro na Zanzibar kwa kile ilichodai kuwa Kenya iliiwekea vikwazo mbalimbali vya kibiashara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!