Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Katiba mpya hiyoo! Samia aagiza Msajili kuitisha kikao maalumu
Habari za Siasa

Katiba mpya hiyoo! Samia aagiza Msajili kuitisha kikao maalumu

Spread the love

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amemuagiza Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi kuitisha kikao maalum cha Baraza la vyama hivyo pamoja na kuanza mchakato wa Katiba Mpya, Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Rais Samia ametoa maagizo hayo jana tarehe 6 Mei 2023 Ikulu , Chamwino, Dodoma ambapo amemtaka Jaji Mutungi kuitisha kikao hicho kwa lengo la kufanya tathmini utekelezaji mapendekezo ya Kikosi Kazi kilichokuwa kikiratibu maoni ya watu kuhusu demokrasia ya Vyama vingi vya siasa nchini.


Mbali na Jaji Mutungi kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na:-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Jenista Mhagama, Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Damas Ndumbaro, Watendaji wa Taasisi mbalimbali.

Katika kikao hicho Rais Samia, ametoa maelekezo ya namna  ya kushirikisha wadau mbalimbali na hasa ushirikishwaji wa Wananchi katika mchakato huo kutoka pande zote mbili Tanzania Bara na Zanzibar.

Mambo mengine yaliyojadiliwa ni pamoja kupitia sheria ya uchaguzi na ile ya vyama vya siasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

error: Content is protected !!