CHAMA cha ACT Wazalendo kimeunga mkono na kuikaribisha kwa mikono miwili hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan kumuagiza Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kuitisha kikao maalum cha Baraza la Vyama vya Siasa nchini kwa ajili ya kutathmini utekelezaji wa mapendekezo ya Kikosi Kazi cha kuratibu maoni ya wadau kuhusu demokrasia ya vyama vingi nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana tarehe 7 Mei 2023 na Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu, imekuwa ni rai ya chama hicho kuhitaji ratiba ya utekelezaji wa mapendekezo ya kikosi kazi.
Amesema wanatarajia kikao hicho kitapatiwa ratiba hiyo ambayo itahakikisha kuna Sheria Mpya ya Uchaguzi na Sheria Mpya ya Vyama vya Siasa kabla ya mwisho wa mwaka huu.
“Vilevile kuhakikisha kwamba mabadiliko ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba yanafanyika ili kuanza mchakato wa Katiba Mpya kwa kuundwa kwa Timu ya Wataalam (Committee of Experts) kana ilivyopendekezwa na kikosi kazi.
“Ni mategemeo ya Chama chetu kuwa Baraza la Vyama vya Siasa itakuwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa Kitaifa ili kujadili mambo yaliyokwamisha mchakato wa Katiba wa 2014 na kupata mwafaka kwayo ili mchakato wa sasa usikwame,” amesema.
Leave a comment