Tuesday , 23 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Polisi wachunguza kifo cha mwanamke anayehusishwa katika ajali ya Naibu Waziri
Habari Mchanganyiko

Polisi wachunguza kifo cha mwanamke anayehusishwa katika ajali ya Naibu Waziri

Spread the love

JESHI la Polisi nchini limeanza uchunguzi wa kifo cha mwanafuzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom),  Nusura Hassan Abdallah kinachodaiwa kutokana na kipigo kutoka kwa mpenzi wake mkoani Kilimanjaro. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Hatua hiyo imekuja baada ya kifo hicho kuhusishwa na ajali illiyotokea jijini Dodoma tarehe 26 Aprili 2023 na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi (Afya), Dk Festo Dugange.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania, David Misime iliyotolewa jana Jumamosi 6 Mei 2023, imesema taarifa za kifo cha Nusura zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai alikuwa mmoja wa majeruhi kwenye ajali hiyo ya Naibu waziri iliyotokea Dodoma.

“Polisi Mkoa wa Kilimanjaro baada ya kuona taarifa hizo kupitia mitandao ya kijamii na sababu zinazotolewa, wameshaanza uchunguzi kwa watu mbalimbali, hospitalini alikotibiwa binti huyo ambapo amesema wanashirikisha Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na wadau wengine wa haki jinai,” inasema sehemu ya taarifa ya Polisi.

Jeshi hilo limetoa wito kwa mtu yeyote mwenye taarifa zilizosahihi na zenye ukweli asisite kutoa taarifa hizo ili kuharakisha uchunguzi wa tukio hilo.

Kwa mujibu wa Misime uchunguzi wa tukio hilo ukikamilika taarifa kamili ya kilichobainika kitatolewa kwa umma na kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa 12 wa kilo 726.2 za dawa za kulevya wafikishwa mahakamani

Spread the love  WATUHUMIWA watatu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari Mchanganyiko

GGML yasisitiza kuendelea kuimarisha afya za wafanyakazi

Spread the loveKAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited kwa kushirikiana na kampuni...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

error: Content is protected !!